Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:15

Baraza la Wawakilishi huenda likamfungulia mashtaka Trump kumuondoa madarakani


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Juhudi za kumwajibisha Rais Donald Trump kutokana na kuhusika kwake na uchochezi wa kulishawishi genge lililovamia Bunge la Marekani Jumatano zimeshika kasi siku ya Jumamosi, ambapo wabunge wa chama cha Democratic katika Baraza la Wawakilishi la Marekani wakitangaza watapendekeza vifungu vya kumuondoa madarakani mapema ifikapo Jumatatu.

Mwakilishi Ted Lieu
Mwakilishi Ted Lieu


Mwakilishi, Mdemokrat kutoka jimbo la California, aliyesaidia kuandaa rasimu ya mashtaka dhidi ya Trump, alituma ujumbe wa Twitter Jumamosi mchana kuwa vifungu vya kumfungulia mashtaka Trump vimeungwa mkono na wawakilishi 180, japokuwa hakuna Mrepublikan aliyeshiriki.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi na wenzake wanahamu kuona rais akiondolewa madarakani kabla ya muda wake kumalizika Januari 20 pamoja na kuwa Baraza la Seneti linaloongozwa na Warepublikan sio rahisi kukubaliana na hatua hiyo.

Spika Nancy Pelosi
Spika Nancy Pelosi

“Mazingira ya huyu rais asiyeweza kudhibitiwa ni hatari zaidi, na lazima tufanye kila tunaloweza kuwalinda wananchi wa Marekani kutokana na mashambulizi yake yasiyokuwa na msingi dhidi ya nchi yetu na demokrasia yetu.”

Iwapo Baraza la Wawakilishi litamfungulia mashtaka rais kumuondoa madarakani, kwa mara ya pili, hilo litapelekea kesi itakayo endeshwa na Baraza la Seneti, ambalo lilimuachia huru Trump mara moja huko nyuma na litakuwa mapumzikoni hadi Januari 19 na baadae Baraza la Seneti litadhibitiwa na Wademokrat baadae mwezi huu.

Viongozi wa Democrat katika bunge pia wamemtaka Makamu Rais Mike Pence kutumia kifungu cha 25 cha Katiba, kinachotoa njia mbadala na pengine ya haraka zaidi kumuondoa rais madarakani. Pence hakuwapa jibu lakini amewaambia wenzake hapendelei hatua hiyo kuchukuliwa.

Makamu wa Rais Mike Pence
Makamu wa Rais Mike Pence

Sheria hiyo iliyopitishwa mwaka 1960, kifungu hicho cha 25 cha Katiba ya Marekani kinaruhusu kukabidhi madaraka kwa muda kutoka kwa rais kwenda kwa makamu wa rais iwapo rais hawezi kutekeleza majukumu yake, kwa idhini ya waliowengi katika Baraza la Mawaziri. Lakini wachambuzi wanasema fursa hiyo inaweza kuwa vigumu kuitekeleza wakati utawala wa Trump umebakiza siku chache.

XS
SM
MD
LG