Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:21

Vitisho vyaongezeka dhidi ya wabunge wa Marekani


Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi
Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi

Wabunge kadhaa wa Marekani hivi karibuni wamepokea vitisho kwa maisha yao, wakati Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi akitaka usalama uimarishwe katika Bunge la Marekani na kudai kuwa kuna hatari inayokuja siyo tu kutoka uraiani lakini kutoka kwa “adui wa ndani” ya Bunge lenyewe.

Madai ya Pelosi Alhamisi yameonyesha kuongezeka kwa mvutano kati ya vyama vya siasa Bungeni juu ya tishio la usalama tangu uvamizi wa mwezi huu ndani ya Bunge uliofanywa na wafuasi wa Rais wa zamani Donald Trump, watu watano waliuawa kufuatia ghasia hizo.

FILE - Genge la wafuasi wa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump fight wakiwashambulia maafisa wa polisi wanaolinda Bungeni walipovami jengo la Bunge la Marekani Washington, Jan. 6, 2021.
FILE - Genge la wafuasi wa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump fight wakiwashambulia maafisa wa polisi wanaolinda Bungeni walipovami jengo la Bunge la Marekani Washington, Jan. 6, 2021.

Zaidi ya wabunge 30 walisaini barua wiki hii iliyotaka wapatiwe ulinzi zaidi katika wilaya zao. Walieleza kuwa vitisho dhidi ya wabunge vimeongezeka sana katika miaka ya karibuni, na takriban vitisho 4,900 vilitolewa katika mwisho wa mwaka wa fedha unaoishia Septemba 2018. Ukilinganisha na vitisho zaidi ya 900 vilivyotolewa mwaka 2016.

Polisi katika Bunge la Marekani wanasema wanachukua hatua kuwalinda wabunge wanapokwenda na kutoka kazini, kwa mujibu wa barua pepe ya Afisa Mkuu wa Polisi Bungeni ambayo shirika la habari la The Associated Press iliipata.

Timothy P. Blodgett, kaimu askari msimamizi wa bungeni, ameandika katika barua pepe kuwa jeshi la polisi linaweka mawasiliano maalum na wabunge, na pia amewasihi kuripoti vitisho au vitendo vinavyotia shaka, wanaweza kuwafahamisha mipango yao ya kusafiri.

Amesema Polisi wa Bunge watawekwa katika maeneo ya viwanja vya ndege na kituo cha Treni cha Union mjini Washington katika siku zenye shughuli nyingi, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

XS
SM
MD
LG