Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:07

Nchi zinazoendelea zaanza kununua chanjo za COVID-19


Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Retno Marsudi alichaguliwa kuwa mwenyekiti mwenza wa kikundi kazi cha COVAX AMC ilioanzishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na ushirika wa Chanjo (GAVI).(Photo: Indonesian Ministry of Foreign Affairs).
Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Retno Marsudi alichaguliwa kuwa mwenyekiti mwenza wa kikundi kazi cha COVAX AMC ilioanzishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na ushirika wa Chanjo (GAVI).(Photo: Indonesian Ministry of Foreign Affairs).

Baadhi ya nchi maskini, zilizo stushwa kuona nchi tajiri zikipokea milioni ya chanjo za COVID-19, zimeamua kutosubiri kupelekewa chanjo kutoka Shirika la Afya Duniani na makundi mengine, na badala yake wameanza kufanya makubaliano yao binafsi kuagiza chanjo hizo.

Juan Carlos Sikaffy, rais wa Baraza la Biashara Binafsi Honduras, ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa Honduras “haiwezi kusubiri mchakato unaofuata urasimu au maamuzi yanayo potoshwa” kuwapatia wananchi “hali ya utulivu” kwa kuwapatia chanjo ya COVID-19

Baraza la Biashara Binafsi Honduras limeshiriki katika kufikia makubaliano ya kununua chanjo kwa taifa hilo la Amerika ya Kati kwa kutoa dhamana ya benki.

Serbia pia imefuatilia yenyewe chanjo iliyoko katika soko pamoSja na kuwa tayari imepokea euro milioni 4 kwa programu ya COVAX ya Shirika la Afya Duniani (WHO), iliyoundwa kusambaza chanjo za COVID kwa uwiano unaotakiwa.

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic alisema hawezi kusubiri COVAX baada ya kuona nchi tajiri zikinunua idadi kubwa ya chanjo hizo muhimu.

“Inaonekana kana kwamba wanakusudia kuwachanja paka na mbwa wao wote pia,” alisema.

Tedros Adhanom Ghebreyesus
Tedros Adhanom Ghebreyesus

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani amezitaka kampuni za kutengeneza dawa siku ya Ijumaa kuruhusu matumizi ya viwanda vyao ili kuongeza uzalishaji wa chanjo za COVID-19.

Akizungumza kwa njia ya mtandao kutoa taarifa kutoka Geneva, Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema kinacho hitajika ni “kuongeza uzalishaji kwa wingi.”

Ameeleza kuwa kampuni ya Ufaransa Sanofi imetangaza itaruhusu miundo mbinu ya kiwanda chake kusaidia katika uzalishaji wa chanjo ya Pfizer/BioNTech na kuzitaka kampuni nyingine kufanya hivyo pia.

“Tuna vishawishi viwanda vyote kushirikiana katika matumizi ya takwimu na teknolojia zao kuhakikisha chanjo inapatikana kwa wote.”

Pia amerejea wito wake kwa nchi tajiri kutoa dozi za chanjo kwa nchi maskini watakapo kuwa wamemaliza kuwachanja wafanyakazi wa afya na wazee.

XS
SM
MD
LG