Kampuni kubwa duniani zinatongeneza chanjo za COVID-19 zinashughulika kwa haraka kutizama kama dozi za chanjo zao zinafanya kazi dhidi ya aina mpya ya virusi vya corona vilivyogunduliwa Uingereza na Afrika kusini.
Chanjo ya COVID-19 ya kampuni ya Pfizer na mshirika wake BioNTech inaonekana kufanya kazi dhidi ya aina mpya ya virusi vinavyoambukiza kwa haraka vilivyogunduliwa uingereza na Afrika kusini, kwa mujibu wa utafiti wa kimaabara ulioendeshwa na kampuni ya marekani ya Pfizer.
“Aina mpya ya ya virusi huko Afrika kusini inawatia hofu wataalamu kwa sababu inawezekana chanjo isijibu kwa njia moja ama nyingine au isifanye kazi kwa njia moja ama nyingine”, waziri Shappys ameiambia radio LBC ya Uingereza.