Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:56

Afrika Kusini yaongeza masharti Jimbo la Cape kudhibiti COVID-19

Watu wakijitolea kupewa chanjo ya AstraZeneca katika kituo cha majaribio cha Hospitali ya Soweto's Chris Sani Baragwanath nje Johannesburg, Afrika Kusini, Jumatatu Nov. 30, 2020. Zaidi ya raia 2000 wa Africa Kusini wamejitokeza kushiriki katika majaribio hayo.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameongeza masharti katika jimbo la mashariki la Cape ambalo limekuwa na ongezeko la maambukizi ya COVID – 19.

Rais Cyril Ramaphosa
Rais Cyril Ramaphosa

Rais ametangaza masharti ya kutotoka nje usiku katika wilaya ya fukwe ya mashariki ya Nelson Mandela Bay ambayo ni kitovu kipya cha maambukizo hayo.

Matumizi ya pombe katika maeneo ya umma kama vile kwenye fukwe yamezuiwa kuanzia Alhamisi katika hatua ambayo rais anasema itapunguza watu kukutana.

Idadi ya watu wanaoruhusiwa katika shughuli za ndani pia imepunguzwa na kuwa 100 wakati watu 250 wataruhusiwa kwa shughuli za nje.

Rais Ramaphosa amewataka watu kufuata masharti hayo yaliyowekwa ili kuzuiya kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona.

XS
SM
MD
LG