Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:21

FAO : COVID-19 yaongeza umaskini na njaa barani Afrika


Wanawake wa kabila la Turkana na watoto wao wakisubiri kugawiwa chakula cha msaada karibu na kambi ya wakimbizi ya Kakuma, Wilaya ya Turkan, kaskazini magharibi ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi, August 8, 2011.
Wanawake wa kabila la Turkana na watoto wao wakisubiri kugawiwa chakula cha msaada karibu na kambi ya wakimbizi ya Kakuma, Wilaya ya Turkan, kaskazini magharibi ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi, August 8, 2011.

Janga la virusi vya corona limeongeza umaskini na njaa kwa watu wengi zaidi mwaka 2020, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO).

Sehemu nyingi barani Afrika, ambako kuna mizozo na mabadiliko ya hali ya hewa tayari wako katika hali mbaya sana.

FAO inasema katika juhudi zake za kupambana na njaa imerudishwa nyuma kwa miaka 10 kwa sababu ya janga la virusi vya corona.

Mchumi mkuu wa FAO, Maximo Torero Cullen anasema tatizo siyo ukosefu wa chakula, lakini fursa ya kukipata.

“Watu hawana fursa ya kupata chakula kwasababu wamepoteza ajira zazo, kwasababu hawana mapato mengine, nchi zinazoendelea zitakabiliwa na changamoto nyingi kwasababu ya hali ya kudorora kwa uchumi duniani, na hivyo hiyo inaelezea kwanini suala la lishe duni litaongezeka mpaka milioni 132,” Cullen anasema. Anatabiri kuwa umaskini nao utakuwa mbaya sana.

“Tunatarajia ongezeko la umaskini kufikia mpaka watu milioni 150 zaidi ambao wataingia katika umaskini uliokithiri; tunaratajia kuwa watu milioni 132 watakuwa na matatizo ya lishe duni,” mchumi mkuu wa FAO anasema.

Walio katika mazingira hatarishi Cullen anasema ni wale walio katika hali ya ghasia au mabadiliko ya hali ya hewa.

Barani Afrika chini ya jangwa la Sahara, katika eneo la Sahel wengi wao tayari wanakabiliwa na mizozo, wengi wao wamekumbwa pia na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa. Au wanakabiliwa na tatizo la uvamizi wa nzige, ambalo limejitokeza sana katika maeneo ya Afrika Mashariki, Cullen ameongezea.

Afrika Mashariki imeona mlipuko mkubwa wa uvamizi wa nzige mwaka huu. Nchini Kenya, iliona athari mbaya za wadudu hao kuwa kuonekana katika kipindi cha miaka 70 wakiingilia maisha ya mamilioni ya watu.

Ingawaje janga COVID-19 limepiga vibaya baadhi ya maeneo ya dunia, kama vile Marekani na Ulaya, utafiti uliofanywa na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imebaini kuwa maeneo ya Afrika yamekuwa na athari tangu kuanza kwa janga hilo.

Halimatou Amadou wa ICRC aliiambia VOA kutoka kwamba utafiti uliofanywa mkiongoni mwa watu 2,400 katika nchi 10 za Afrika, na wale waliohojiwa wanasema hali inatisha.

Kwa mfano, asilimia 94 ya watu hao wameieleza ICRC kwamba bei za vyakula zimeongezeka katika masoko ya ndani. Pia wameona kwamba asilimia 82 ya watu waliohojiwa wakisema wamepoteza mapato au ajira.

Amadou anasema ni asilimia 7 tu ya watu hao wamesema walikuwa na akiba ya kutosha kukabiliana na hali ya sasa. Katika sehemu nyingine, hali imezidi kuwa mbaya kwasababu ya mizozo.

Nchini Burkina Faso, kiasi cha watu milioni 8 wanakabiliwa na ukosefu wa chakula au hali mbaya kuliko hiyo. Kwa hakika asilimia 200 zaidi kuliko mwaka 2019.

Tulichokiona anasema Amadou ni kwamba hivi sasa kuna watu zaidi ya milioni moja ambao wamekoseshwa makazi na wale ambao hawana fursa ya ardhi ya kilimo. Kwa kawaida hiyo imefanya hali kuwa ngumu zaidi kwa wao kupata chakula.

Mbali ya Afrika, FAO ina wasi wasi mkubwa na eneo la Amerika Kusini, ambalo limepigwa vibaya sana na COVID-19.

XS
SM
MD
LG