Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 00:59

Mataifa ya Afrika Mashariki yatakiwa kuendelea kuwapokea wakimbizi


Amnesty International
Amnesty International

Mataifa ya Afrika Mashariki yametakiwa kufungua milango yao kuwapokea wakimbizi kutokana na kuendelea kwa mizozo nchini Somalia, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo licha ya kuwepo kwa janga la COVID-19, Ushirika wa jumuiya za wakimbizi katika Pembe ya Afrika, Afrika Mashariki na Afrika ya Kati (HECA) imesema.

Deprose Muchena, mkurugenzi wa Amnesty International kwa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, amesema kuwa wakati nchi katika eneo hilo zinakabiliwa na uhalisia wa hali ya dharura ya afya ya umma, nchi zenye kupata misaada kutoka kwa washirika wa kimataifa lazima zitafute ufumbuzi ambao utaheshimu haki za kimataifa za binadamu na kutekeleza kwa dhati sheria za wakimbizi, ikiwemo haki ya kuomba hifadhi.

“Serikali inatakiwa ifikirie hatua mbalimbali kama vile upimaji wa COVID-19, tahadhari na eneo la kuwaweka karantini wakimbizi katika eneo la mpakani ili kuwawezesha kuomba hifadhi katika nchi hizo,” amesema Muchena katika taarifa ya pamoja iliotolewa Juni 22.

HECA, ambayo inajivunia kwa kuwa na wanachama 39, inaitaka Kenya, Uganda, Sudan, Rwanda na Tanzania kufungua mipaka yake kwa wanaoomba hifadhi. Burundi, Ethiopia, Rwanda na Somalia walifunga mipaka yao mwezi Machi. Nchini Kenya, mipaka kati yake na Somalia na Tanzania ilifungwa Mei 16.

Hivi sasa, maelfu ya wakimbizi wamekwama katika mipaka kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Uganda na Sudan Kusini; Kenya na Somalia, na Kenya na Sudan Kusini.

HECA inasema kuwa ufungaji wa jumla wa mipaka unakiuka sheria ya kimataifa ya wakimbizi kwani ni kuwanyima watu wenye shida nzuri msaada wa kimataifa ikiwa ni fursa ya kuwasaidia wale wanaoomba hadhi ya ukimbizi.

XS
SM
MD
LG