Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 09:41

UNHCR: idadi ya wakimbizi yafikia milioni 79 duniani, wakati msaada wapunguka


FILE - Watoto wakimbizi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiandikishwa kuchukuliwa katika makazi ya Kyangwali magharibi mwa Uganda, December 10, 2018.
FILE - Watoto wakimbizi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiandikishwa kuchukuliwa katika makazi ya Kyangwali magharibi mwa Uganda, December 10, 2018.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR linaeleza wasi wasi kutokana na kuongezeka idadi ya wakimbizi duniani kwa milioni 9 mnamo mwaka wa 2019, pekee yake. 

Kamishna wa UNHCR Filippo Grande anasema hiyo ni idadi ya kutia wasi wasi, kwani hivi sasa idadi ya waklimbizi na walokoseshwa makazi duniani imefikia milioni 79 ambapo wengi kati ya hao ni wale walobaki ndani ya nchi zao na miloni 29.9 kati ya hao nidio wakimbizi nje ya nchi zao.

Hiyo ndio idadi kubwa kabisa ya wakambizi kuwahi kuorodheshwa ikiwa ni asili mia 1 ya wakazi wa dunia hivi sasa.

Dunia inaandhimisha June 20, kama siku ya wakimbizi ambapo mwaka huu kauli mbiu ni, “Kila hatua ni muhimu.” Kila mtu anaweza kuleta tofauti katika maendeleo ya dunia, na hivyo kuwashirikisha katika jamii wanakoishi ni muhimu.

Juhudi za kuwashirikisha wakimbizi katika jamii zimekua zikendelea Uganda na Rwanda kwa muda mrefu kutokana na kwamba nchi hizo hazina sera ya kuunda kambi za wakimbizi.

Nchini Uganda wakimbizi wanaruhusiwa kuishi mijini na kusaidiwa kupata ajira katika jamii inayowapokea na kuweza kuendelea pia na masomo bila ya kubaguliwa.

Kenya na Tanzania zenye sera za kuwaweka kambini wakimbizi, hazijaitikia wito wa kuwawezesha wakimbzi kuweza kukidhi mahitaji yao ya maisha kwa kufanya kazi.

Hata hivyo Shirika la UNHCR na lile la Kazi Duniani ILO zinafanya juhudi kutoa mafunzo ya kazi kwa wakimbizi kwenye kambi kubwa ya wakimbizi duniani Daadab, ili kuweza kupata ajira na kujitegemea.

XS
SM
MD
LG