Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 13:56

Zoezi la uhakiki wa raia wa Kenya wanaokana sio wakimbizi waanza


Kambi ya Dadaab, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia Agosti 29, 2011.
Kambi ya Dadaab, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia Agosti 29, 2011.

Zoezi la kuwakagua raia wa Kenya walioingia katika kumbukumbu za shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi, UNHCR, imeanza katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab.

Kwa mujibu wa serikali ya Kenya zaidi ya wa Kenya elfu 40 walijisajili kama wakimbizi ilikupokea msaada wa chakula , dawa na hata elimu baada ya maeneo ya kaskazini mashariki mwa kenya kukumbwa na tishio la baa la njaa .

Miaka ya 90 baada ya baa la njaa kulikumba eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya raia wengi wa Kenya walijiingiza kuwa wakimbizi baada ya UNCHR kuwasajili katika kambi ya Dadaab. .

Ukosefu wa chakula ni tishio la magonjwa na elimu. Raia hawa pia walikuwa wananyemelea fursa ya kupata uraia katika mataifa ya magharibi na hivyo wazazi wengi ambao ni raia wa kenya walijisajili kama wakimbizi.

Asha Shurie Abdi mkazi wa Dadaab ni miongoni mwa wazazi waliosajili wanawe kama wakimbizi ili kunufaika na yale wakimbizi wanayostahili kupokea kama msaada.

Shurie hakujua maisha ya wanawe yangebadilika kuwa ni wakimbizi, uamuzi amabo umewanyima wanawe kupata stakabadhi muhimu kama vile kitambulisho na hata kukosa kazi licha ya kumaliza chuo kikuu

Siyo tu familia hiyo ni zaidi ya raia elfu 40 ni wakimbizi licha ya wao kuwa ni Wakenya.

Wakati zoezi la kuwa ondoa katika data ya UNCHR ilipoanza mjini dadaab maelfu walijitokeza idadi kubwa ikiwa ni wanawake na vijana .

Abdullahi Mohamed yuko mbio kumsaidia mkewe raia wa Kenya ila yupo katika kumbukumbu za usajili wa wakimbizi wa UNHCR.

Mohamed anasema kabala ya kumuoa , mkewe alikuwa anajaribu bahati yake kusaka maisha mazuri ughaibuni

Kwa mujibu wa naibu kamishan eneo la dadaab Hussein Abdirahman anasema zoezi litachukua muda mrefu kutambua wakenya halisi

Naibu Kamishna huyo amesema waliofikia kutoka katika kumbukumbu za UNHCR walilazimika kuwaleta wazazi wao walio na vitambulisho vya kenya, viongozi wa maeneo wanayotoka ilikutambua iwapo wanasema ukweli .

“Ukweli ulianza kuzama kwa wakazi wa dadaab baada ya serikali kupanga kufunga kambi ya Dadaab na huduma kama hospitali, shule na shamba kukabidhiwa serikali ya Kenya na zoezi la kurudi somalia likaanza ....... kilichosalia sasa kwa wakzi hao ni kusubiri iwapo matokea yatathibitisha wao ni Raia wa Kenya.

Imeandaliwa na Mwandishi wetu Huba Abdi, Kenya

XS
SM
MD
LG