Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 16:35

Kagame asema Rwanda itaanza kupokea wakimbizi kutoka Libya


Rais wa Rwanda, Paul Kagame akizungumza kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini New York. Septemba 24, 2019.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame akizungumza kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini New York. Septemba 24, 2019.

Rais Paul kagame wa Rwanda alitoa matamshi hayo kwenye hotuba yake ya Jumanne kwa wajumbe wa kikao cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York . Mkutano ambao hufanyika kila mwaka na kujadili masuala mbali mbali ikiwemo usalama, afya, elimu, mabadiliko ya hali ya hewa na mengineyo

Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema nchi yake itaanza hivi karibuni kupokea wakimbizi kutoka nchini Libya kufuatia makubaliano waliyofikia kati ya serikali yake na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi-UNHCR.

Kagame ni miongoni mwa viongozi wa mataifa Duniani wanaohudhuria kikao cha kila mwaka cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York nchini Marekani.

Sauti ya Amerika-VOA ilifanya mahojiano na mtangazake wake Idd Ligongo anayehudhuria mkutano huo na kumuuliza masuala gani mengine ambayo Rais Kagame amayazungumza katika hotuba yake kwenye Umoja wa Mataifa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:34 0:00

Wakati huo huo Rais wa Marekani, Donald Trump akiwa kwenye mkutano huo wa Umoja wa Mataifa alisema kwamba wakati ambapo Marekani haitaki mzozo na taifa jingine lolote, haitosita kulinda maslahi ya Marekani. Rais Trump alizungumzia utawala wa Iran kama moja ya vitisho vikubwa sana Duniani akisema utawala unakandamiza raia wake nyumbani huku ikichochea mizozo na ugaidi nje ya mipaka yake.

Rais Donald Trump wa Marekani
Rais Donald Trump wa Marekani

Alisema iwapo hili linaendelea vikwazo vya Marekani havitaondolewa na vitaimarishwa. Lakini Rais huyo wa Marekani aliacha mlango wazi wa kidiplomasia akieleza kuwa baadhi ya maadui wa zamani wa Marekani hivi sasa ni marafiki wa karibu sana na Marekani.

XS
SM
MD
LG