Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 16:35

Magufuli awataka wakimbizi walioko Tanzania kurejea makwao


Rais John Magufuli
Rais John Magufuli

Rais wa Tanzania John Magufuli amesema Ijumaa, wakimbizi walioko nchini Tanzania lazima warejee makwao, wiki moja baada ya maafisa kuanza kuwarudisha makundi ya raia wa Burundi pamoja na kuwepo wasiwasi kuwa wanaweza kukabiliwa na ukandimizaji wa kisiasa.

Maafisa wa Tanzania walikuwa wamesema watakaorejeshwa wataondoka kwa hiari yao, lakini Magufuli ameonya katika hotuba yake kuwa wakimbizi nchini Tanzania, wengi wao kutoka Burundi, hawawezi kubakia milele na hawatapatiwa uraia.

“Rudini makwenu… msisitize kubakia Tanzania kama wakimbizi au kutegemea kupatiwa uraia wakati Burundi inautulivu,” Magufuli amesema wakati wa mkutano wa hadhara katika mkoa wa Katavi karibu na kambi kubwa ya wakimbizi upande wa kaskazini magharibi ya Tanzania.

“Hata Yesu alikimbilia Misri kama mkimbizi… na akarejea nchini kwake kuhubiri. Kwa nini mnataka kubakia Tanzania moja kwa moja badala ya kurejea katika nchi yenu?” amesema.

Wananchi wa Burundi ambao ndiyo waliowengi kati ya wakimbizi 280,000 waliosajiliwa nchini Tanzania mwisho wa mwaka 2018, kwa mujibu wa taarifa za Umoja wa Mataifa (UN).

Mamia ya wananchi wa Burundi wameuawa katika mapigano kati ya vikosi vya usalama vya serikali tangu mwaka 2015, wakati Rais Pierre Nkurunziza alipogombea nafasi ya urais kwa muhula wa tata uliokuwa na utata.

Burundi na Tanzania zilikubaliana Agosti kuwarejesha makwao takriban wakimbizi 200,000 ambao walikuwa wameomba hifadhi nchini Tanzania.

Operesheni ya kuwarejesha wakimbizi hao ilianza wiki iliyopita, huku baadhi ya wakimbizi wakieleza hofu yao kuwa huenda wakalazimishwa kurejea makwao baada ya kuwa walihakikishiwa na serikali zote mbili ya Burundi na Tanzania na Umoja wa Mataifa kuwa hawatalazimishwa kuondoka.

Burundi inakaribia kufanya uchaguzi mwaka 2020. Vyombo vya usalama vinaendelea kuwatesa, kuwabaka na kuwaua wananchi ambao wanadhania wanampinga Nkurunziza, UN iliripoti mwezi Septemba.

XS
SM
MD
LG