Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:20

UNHCR : Hali bado siyo shuwari kwa wakimbizi kurejea Burundi


Wakimbizi wakisubiri maji katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kaskazini mwa Tanzania, Mei 28, 2015.
Wakimbizi wakisubiri maji katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kaskazini mwa Tanzania, Mei 28, 2015.

Wakati hali ya usalama kwa ujumla imeboreshwa, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR) linamaoni kuwa hali nchini Burundi bado siyo shuwari hivi sasa kuweza kushawishi wakimbizi kurejea nyumbani.

Taarifa iliyotolewa na UNHCR Alhamisi inasema kuwa shirika hilo linaendelea kuwasaidia wakimbizi ambao wameeleza kuwa wamefanya uamuzi wao binafsi wakiwa huru na kuwa na taarifa za kutosha katika uamuzi wao wa kurejea makwao kwa hiari zao.

Takriban wakimbizi 75,000 wamesharejea nchini Burundi tangu Septemba 2017, wakieleza matakwa yao ya kurudi majumbani kwao na mashambani na kuungana na familia zao.

UNHCR imetoa wito kwa serikali hizo mbili za Burundi na Tanzania kutekeleza ahadi ya jukumu la kimataifa na kuhakikisha kuwa wakimbizi wanaorejea makwao wanafanya hivyo kwa hiari yao kwa kufuata makubaliano ya pande tatu yaliyosainiwa Machi 2018.

UNHCR inazitaka serikali kuhakikisha kuwa hakuna mkimbizi anayerejeshwa Burundi kinyume cha matakwa yake, na kuwa hatua zichukuliwe kufanya hali ya usalama kuwa shuwari kwa wakimbizi wanaorejea, ikiwemo juhudi za kuwajengea imani na kuwapa motisha wale wanaochagua kurudi makwao.

Wakati huohuo, mamia ya Warundi wanaendelea kukimbia kutoka Burundi kil mwezi, na UNHCR inazitaka serikali katika eneo kufungua mipaka yake na kuwawezesha wale wanaotaka hifadhi katika nchi hizo kufanya hivyo.

Pia inatafuta fedha kwa ajili ya kuwasaidia zaidi ya wakimbizi 400,000 na kuwasaidia wale wanaotaka kurejea kuungana na familia zao Burundi na wale ambao wanatarajiwa kurejea kwa hiari yao mwaka 2019.

XS
SM
MD
LG