Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 18:20

Burundi iko katika wimbi jipya la ukatili - Ripoti ya UN


Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

Burundi imeelezewa kuwa iko katika hatari ya wimbi jipya la vitendo vya ukatili wakati taifa hilo likiwa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao wa 2020.

Hayo yameelezwa katika ripoti ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa. Wakati huo huo ripoti iliyotolewa Jumatano inaeleza kuwa mzozo wa kisiasa unaolikabili taifa hilo bado haujapatiwa ufumbuzi,

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters ripoti hiyo inasema kuna hali ya khofu na manyanyaso dhidi ya mtu yoyote ambaye haonyeshi kuunga mkono chama tawala cha CNDD- FDD.

Polisi, majeshi ya usalama na kitengo cha vijana katika chama tawala maarufu kama Imbonerakure wameendelea na ukiukaji mkubwa sana wa haki za binadamu, ikiwemo mauaji, watu kupotea, mateso na ubakaji wa magenge unaofanywa dhidi ya watu wanaompinga rais Pierre Nkurunziza.

Wachunguzi wamesema vigezo vyote nane walivyoainishwa katika ripoti ni mambo ambayo yanatokea hivi sasa nchini Burundi.

Mweneyekiti wa jopo hilo la uchunguzi, Doudou Diene amesema katika taarifa yake kwamba hakuna onyo zuri la mapema kuliko hili.

Ripoti pia imezungumzia kuongezeka kwa udhibiti wa serikali kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na pia hakuna mfumo wa kweli wa vyama vingi vya kisiasa nchini, kwa vile juhudi za serikali za kuviingilia na kuvigawanya.

Pia ripoti imesema kuwa rais Nkurunziza amejiongezea nguvu kubwa kimadaraka, na kufanya uteuzi ambao hauendani na mamlaka aliyonayo kikatiba na kutegemea miundo isiyo rasmi kama vile kamati ya majenerali.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG