Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 26, 2024 Local time: 20:54

Ripoti : Uhuru wa raia waminywa katika baadhi ya nchi za Kiafrika


Hatua za ukandamizaji dhidi ya asasi za kiraia Afrika tangu mwaka 2004
Hatua za ukandamizaji dhidi ya asasi za kiraia Afrika tangu mwaka 2004

Nchi 12 barani Afrika, zikiwemo Tanzania, Burundi, Uganda, zimepitisha sheria au sera “zinazokandamiza kimakosa” asasi zisizokuwa za kiserikali na jumuiya za kiraia ambazo ziko hatarini, imeeleza taasisi inayofuatilia demokrasia, Freedom House, katika ripoti yake mpya.

"Vikwazo dhidi ya NGOs vinaathiri uwezo wa jumuiya za kiraia kujipanga, na raia, kuweza kuziwajibisha serikali na kusimamia haki za binadamu,” amesema Godfrey M. Musila mwandishi wa ripoti iliyotolewa Jumanne na Taasisi inayojitegemea yenye makao yake Washington.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:16 0:00

Udhibiti wa madikteta au serikali kandamizi

Ameongeza kuwa vipingamizi vilivyowekwa na serikali” bila shaka vinaambatana na hatua nyengine za kuzuia aina nyengine za uhuru” na kuimarisha udhibiti unaofanywa na serikali au mtu anayetawala kwa mabavu.

Ripoti hiyo inaangalia vipingamizi vilivyoanza kuwekwa kwa jumuiya za kiraia tangu mwaka 2004, hususan vikundi vinavyo jishughulisha na haki za binadamu na masuala ya utawala.

Hatua kama vile kuweka ugumu katika usajili au kuzuia wafanyakazi wa kigeni na misaada ya kifedha zimekuwa zikitekelezwa katika nchi zifuatazo : Algeria, Burundi, Misri, Ethiopia, Rwanda, Sierra Leone, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania, Tunisia, Uganda and Zambia. (Ethiopia imeondoa vikwazo hivyo mwezi Februari, 2018.)

Nchi zilizochelewesha kutekeleza

Ripoti hiyo inasema kuwa vikwazo dhidi ya NGO vimewekwa pembeni au vinaweza kutekelezwa nchini Misri, Malawi, Msumbiji, Rwanda, Sudan na Zambia.

Vikwazo kama hivyo vilianzishwa lakini vikatupiliwa mbali na viongozi, vikakataliwa na bunge, au vikafutwa na mahakama katika nchi sita : Kenya, Angola, Congo-Brazzaville, Malawi, Nigeria and Zimbabwe

Ethiopia imepiga hatua kuondoa vikwazo

Ethiopia mwaka 2009 ilikuwa imeweka kile Musila anachokieleza kwa VOA kama ni vikwazo “kandamizi” – kama vile kuzuia makundi ya haki za binadamu kushiriki katika uhamasishaji – lakini iliziondoa baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuchukua madaraka Aprili 2018.

Na katika nchi hii ya Pembe ya Afrika inang’ara. Lakini nyingi kati ya nchi 20 zilizofanyiwa utafiti katika ripoti hii, hatua ziko tayari au zinachukuliwa na sheria zinabadilishwa sio tu kuminya rasilmali za sekta ya jumuiya za kiraia, lakini pia serikali inaweka vizuizi imara zaidi dhidi yao,” amesema Musila.

XS
SM
MD
LG