Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:27

Vipi tunaweza kuienzi Siku ya Radio Duniani?


Vifaa vya kutupia mawasiliano ya radio yaliyokuwa yanatumika Julai 13, 2018, Afrika Kusini.
Vifaa vya kutupia mawasiliano ya radio yaliyokuwa yanatumika Julai 13, 2018, Afrika Kusini.

Leo ni Siku ya Radio Duniani. Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (Unesco) mwaka 2019, linawakumbusha wadau mbalimbali duniani wajitahidi kadri wanavyoweza kusaidia kukuza mazungumzo, uvumilivu na amani (kauli mbiu ya mwaka huu) baina ya jamii na mataifa mbalimbali.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, katika ujumbe wake Jumatano anasema : “Katika Siku ya Radio Duniani, ni juu yetu kutambua nguvu ya radio katika kushawishi majadiliano chanya, kuvumiliana na kuendeleza amani ulimwenguni.

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres

UNESCO ilianzisha Siku ya Radio Duniani mwaka 2011 mara baada ya Baraza Kuu la Unesco kutambua umuhimu wake. Februari 13, 1946, UN ilianzisha Radio ya Umoja huo.

Wachambuzi wa kisiasa wanakubaliana kuwa ni katika kutumia chombo hiki cha mawasiliano na msingi wa kutoa habari radio imekuwa chachu ya kukuza uhuru wa kujieleza na kusukuma mbele haki za binadamu duniani.

Radio ni mawasiliano ya umma ambayo yanawafikia kundi kubwa la wasikilizaji ulimwenguni kote. Bado inatambulika kuwa ni chombo cha mawasiliano chenye nguvu ya ushawishi na kinatumia gharama ndogo zaidi.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa radio iliandaliwa kuzifikia jamii zilizo katika maeneo yaliyoko kando ya miji na vijiji, ambavyo haviwezi kufikiwa kwa urahisi kutokana na matatizo ya barabara na usafiri. Hizi ndizo jamii ambazo zinaathirika zaidi na matatizo mbalimbali. Jamii hizi zinamakundi kama vile, waliokosa fursa za elimu, wenye ulemavu, wanawake, vijana na maskini.

Radio za Kijamii
Radio za Kijamii

Radio imeendelea kuwajulisha watendaji mbalimbali matatizo ya jamii kama hizi tulizozitaja kupitia mijadala mbalimbali na kuwapa fursa viongozi kuchukua hatua. Mijadala hii ya umma, inawaunganisha watu bila ya kujali tofauti zao za kielimu. Pia radio husaidia sana kufikisha ujumbe katika hali za dharura na kuwapa taarifa za matumaini kwa waathirika wa majanga mbalimbali, wakati misaada mbalimbali inapokuwa iko njiani kuwafikia.

Lakini kubwa kuliko yote, kuna sura mpya ya radio hivi katika miaka ya hivi karibuni baada ya mawasiliano mbalimbali kuunganishwa. Radio inatumia aina ya teknolojia mpya kama vile simu za mkononi, vifaa ya elektroniki kama vile Tablet, na mitambo yenye nguvu inayosambaza ujumbe mwingi kwa wakati mmoja kupitia mawasiliano ya broadband.

Mitandao ya Kijamii inavyoweza kukupatia mawasiliano ya radio
Mitandao ya Kijamii inavyoweza kukupatia mawasiliano ya radio

UNESCO inawahamasisha watu kufungua Radio majumbani, kwenye magari au simu za mkononi ili kuenzi chombo hiki maalum ambacho kimesikindikiza maisha ya kila mtu katika historia.

Radio imekuwa ni muhimu katika jamii mbalimbali ikitumika nyumbani, katika gari au simu za mkononi.

Unesco katika ujumbe wake mwaka huu pia imevihimiza vituo vyote vya Radio na mashirika yote ya kidini na umma ulimwenguni, kuunga mkono jitihada zinazoendelea za kuhamasisha wasilikizaji umuhimu wa kuheshimu fikra tofauti na wakati huohuo kuhimiza amani na maendeleo duniani.

XS
SM
MD
LG