Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:53

Mitandao ya Kijamii : Marekani yawatahadharisha raia wake Tanzania


Mitandao ya Kijamii
Mitandao ya Kijamii

Serikali ya Marekani imewatahadharisha raia wake nchini Tanzania kuhakikisha picha zao na hisia zao haziingii katika mitandao hiyo.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa tahadhari hiyo kupitia mtandao wake.

Ubalozi huo umesema iwapo kuna raia wa Marekani atakuwa amekamatwa au kuzuiliwa katika kampeni hiyo ya kuwakamata mashoga, ahakikishe kwamba viongozi wa Tanzania wameutaarifu ubalozi wa Marekani.

Umoja wa Ulaya nao umemwita balozi wake nchini Tanzania huko Brussels, ili awapatie taarifa kuhusu hali halisi ya haki za binadamu inayojiri katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Wakatti huohuo Shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu Amnesty International, linasema kutokana na tamko la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam la kuwasaka mashoga, mashoga wengi wanaishi katika hali ya uoga na wasiwasi.

Naibu Mkurugenzi wa Amnesty International, kanda ya Afrika Mashariki, Seif Magango ameiambia Sauti ya Amerika “ niliwasiliana na wanaharakati wa haki za mashoga nchini Tanzania, wote wame thibitisha kwamba hofu imetanda na kuwa watu wanahofia usalama wao.

XS
SM
MD
LG