Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:19

Tanzania : Kauli ya Makonda dhidi ya ushoga sio msimamo wa serikali


Paul Makonda
Paul Makonda

Serikali ya Tanzania imesema kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ikitangaza kampeni ya kukabiliana na vitendo vya ushoga katika jiji la Dar es Salaam sio msimamo wa serikali.

Katika tamko lake iliotowa Jumapili, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeeleza kuwa kauli ya Makonda ni mawazo yake na sio msimamo wa serikali.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingependa kufafanua kwamba, hayo ni mawazo yake na sio msimamo wa serikali,” limesema tamko hilo.

Aidha, wizara imesema kuwa serikali ya Tanzania ingependa kutumia nafasi hii kukumbusha na kusisitiza kwamba, itaendelea kuheshimu mikataba yote ya kimataifa inayohusu haki za binadamu ambayo imesaini na kuridhia.

Serikali ya Tanzania imesisitiza kuwa itaendelea kuheshimu na kulinda haki hizo kama zilivyo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

XS
SM
MD
LG