Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:43

Magufuli asema hana kipaumbele cha mageuzi ya katiba


Rais Magufuli akizungumza katika Kongamano la hali ya uchumi na Siasa Tanzania
Rais Magufuli akizungumza katika Kongamano la hali ya uchumi na Siasa Tanzania

Rais John Magufuli amesema serikali yake haina mpango wa kuanzisha upya mchakato wa mageuzi ya katiba kwa sababu kuna maswala mengine yenye kipaumbele kwa serikali yake.

"Sitegemei kutenga fedha kwa ajili ya watu kula wakakae bungeni kujadili katiba, hata kama kuna mtu anataka kutupa hizo fedha, atupe tukatengeneze reli. Watu wanakaa wanapiga kelele katiba mpya, utadhani katiba ndio mwarubaini wa kila kitu," amesema Magufuli.

Rais Magufuli alisema hayo katika kongamano la kujadili hali ya siasa na uchumi wa nchi lililojumuisha maprofesa na viongozi kutoka katika sekta mbalimbali za serikali na Jeshi, Alhamisi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Hata hivyo amewataka wale wenye fedha wanaotaka kusaidia mpango huo wampatie ili akamalizie mradi wa kujenga reli mpya ya kisasa na mradi wa Stiegler’s Gorge.

Rais Magufuli amesema hali ya uchumi ya nchi kwa sasa inakuwa kwa asilimia saba na Tanzania ni miongoni mwa nchi Tano za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi na atasimamia hili ili ukuwe zaidi ya hapa.

“Nchi yetu ilifika katika hatua kubwa sana ya rushwa na ndiyo maana niliamua kujipa kazi kubwa ya kutumbua majipu kwa sababu nilitaka kufikisha nchi sehemu nzuri pamoja na changamoto zake niliapa lazima tutafika tu.

“Katika mambo makubwa ya msingi ni lazima tuyasimamie kwa pamoja kama watanzania bila kujali itikadi zetu za kisiasa na vyama na tusikubali kutumiwa,”amesisistiza Magufuli.

XS
SM
MD
LG