Hata hivyo kikao hicho hakikuhudhuriwa na wawakilishi wa serikali ya Burundi
Akizungumza wakati akifungua kikao hicho Rais Mkapa amesema hadi sasa jitihada zake za kuishawishi serikali ya Burundi kuhudhuria kikao hicho hazijafanikiwa.
Lakini amesema mjadala huo utaendelea na ataendelea kutimiza jukumu alilopewa na wakuu wa nchi za Jumuiya ya Arfrika Mashariki
Aidha Mkapa amewataka washiriki wa mazungumzo hayo kuwa huru kujadili na kutoa mapendekezo yao wanayo amini kuwa yataweza kuleta amani ya kudumu katika taifa la Burundi na kuhakikisha kuwav uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020 kuwa ni huru na wa haki .
Mara Baada ya kufungua kikao hicho msuluhishi huyo alisema anatarajia kukutana tena na washiriki hao baada ya siku mbili ili kupokea mapendekezo na maoni yao ambayao atayaweka katika ripoti atakayo iwasilisha kwa wakuu wa nchi za ushirikiano wa Afrika mashariki
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani akiwemo mwenyekiti wa CNDD amesema kutoshiriki kwa serikali ya Burundi kuna wakatisha tamaa ya kupatikana kwa kile walichotarajia
Mgogoro wa kisiasa katika nchi ya Burundi ulianza mwaka 2015 kufuatia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ambao licha ya kuwa ulifanyika hali ya amani, vitisho na vurugu viliendelea kuiandama nchi hiyo hatua iliyopelekea Umoja wa Afrika kuingilia kati na kuagiza jumuiya ya Afrika Mashariki kutatua mgogoro huo .
Baada ya maelekezo hayo ya umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki ilimteua Rais Yoweri Kaguta Museven kuwa msuluhishi mkuu wa mgogoro huo akisaidiwa na Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Benjamini Mkapa .
Kwa mujibu wa Rais Mkapa kikao kinacho endelea ni cha mwisho, lakini kutokana na mapendekezo yaliyo tolewa na wadau katika mazungumzo ya awamu ya nne, Jumuiya ya Afrika Mashariki itaendelea kusimamia maridhiano hayo na kuhakikisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2020 unafanyika kwa uhuru haki na amani.