Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:37

Burundi yatoa masharti kwa mashirika yasiyo ya kiserikali


Burundi map
Burundi map

Serikali ya Burundi imetoa masharti yanayotakiwa kutimizwa na mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali ili yaruhusiwe tena kufanya kazi zake nchini humo.Hii ni baada ya serikali kusimamisha shughuli za mashirika hayo kwa kipindi cha miezi mitatu.

Kati ya masharti mapya ni kuheshimu sheria zinazohusu mashirika ya kimataifa kama kuwaajiri wafanyakazi kutoka makabila yote kwa viwango vinavyoagizwa na katiba ya Burundi.

Hata hivyo shule na hospitali zinazomilikiwa na mashirika hayo zitazidi kufanya kazi

Masharti ya serikali

Waziri wa Mambo ya Ndani Pascal Barandagiye alitangaza masharti hayo katika mkutano na waakilishi wa mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali Jumanne.

Amesema ni masharti manne, la kwanza kuonyesha makubaliano ya ushirikiano kati ya shirika hilo na wizara ya mambo ya nje, kukubali kuheshimu sheria inayohusu utendaji kazi wa mashirika yasiokuwa ya kiserikali ambayo inaagiza makabila yote yaajiriwe kwa viwango vinavyoagizwa na katiba ya Burundi, asilimia 40 ya watutsi ambalo ni kabila la walio wachache na asilimia 60 ya wafanyakazi wawe ni wahutu.

Kuhusu sharti la uwakilishi wa makabila, Waziri Barandagiye amesema litasahihishwa kwa kipindi cha miaka mitatu hatua kwa hatua.

Mashirika hayo pia yanatakiwa kukubali kwamba mipango yao itekelezwe sambamba na mpango wa kitaifa wa maendeleo, yaheshimu utaratibu kuhusu njia inayoagizwa na serikali ya kupta pesa zao.

“shirika ambalo litaonyesha karatasi tulizoomba hata kesho litaweza kufungua milango yake hata kesho asubuhi. Ni kama leo nchini Burundi hakuna hata shirika moja la kimataifa” amesema waziri Barandagiye.

Jibu la mwakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali

Muakilishi wa shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF linalofadhiliwa na nchi ya Ubelgiji, naye ameuliza kuhusu hatma ya shughuli za dharura wanazofanya kama za hospitali ama shule.

waziri Barandagiye anasema hospitali na shule zinazomilikiwa na mashirika ya misaada zitaendelea kufanya kazi.

“Serikali ya Burundi haijasema kamwe shule au hospitali za mashirika ya kimataifa zifungwe, ambaye atafunga hospitali halafu wagongwa wakafa, ataajibika na sio serikali” amesema waziri Barandagiye

Kumekuwepo na hali ya wasiwasi kuwa hospitali na madaktari wasiokuwa na mipaka MSF nchini Bujumbura zitafungwa.

Hospitali zinazosimamiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Burundi huwahudumia mamilioni ya watu mskini.

Idadi ya mashirika yaliyofungwa

Jumla ya mashirika 130 yamefungwa na serikali ya Bujumbura na inakadiriwa kuwa yalikuwa na wafanyakazi wasiopungwa 40000.

Wafanyakazi wameeleza kughadhabishwa na hatua ya serikali kuyafunga mashirika hayo.

Kando na ajira kubwa kwa raia wa Burundi, mashirika yasiyo ya kiserikali huchangia pakubwa katika sekta za kilimo ambayo ndio tegemeo kubwa kwa uchumi wa Burundi.

Imetayarishwa na Haidallah Hakizimana, Sauti ya Amerika, Bujumbura, Burundi

XS
SM
MD
LG