Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:10

Kufungwa NGOs : Matibabu yasitishwa kwa Wakimbizi Burundi


Wakimbizi wa Burundi
Wakimbizi wa Burundi

Wakimbizi wanaoishi nchini Burundi wasema, moja ya madhara ya kusimamishwa kwa muda mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali ( NGOs) ni kuwepo msongamano wa wagonjwa wanaohitaji huduma.

Wakimbizi hao kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC waishio katika kambi moja mashariki mwa Burundi, wanakiri kuwa hatua ya serikali ya Burundi kusitisha shughuli za mashirika ya kimataifa yasio kuwa ya kiserikali imeanza kuleta madhara kambini.

Kambi hiyo inayopatikana katika mkoa wa mashariki mwa Burundi wa Ruyigi inayo wakimbizi zaidi ya elfu 10 kutoka DRC, wengi wao ikiwa kutoka kabila la Wanyamulenge.

Mwakilishi wa wakimbizi

Mwakilishi wa wakimbizi hao, Freddy Gakunzi ameiambia Sauti ya Amerika Alhamisi kulikuwa na msongamano wa wagonjwa lakini wengi hawakupata matibabu.

“Shirika la Kitaliano (GVC) ambalo linatoa huduma ya afya, sasa limeanza kutoa huduma za dharura tu. Wafanyakazi wa shirika hilo wameonekana wakiwa wachache kambini, hata daktari hakuoenekana,” amesema Gakunzi.

Watoto wakosa uji

Ameongeza kuwa, watoto wengi wanao sumbuliwa na utapiamlo, hawakupewa uji kama ilivyokuwa hapo awali.

Gakunzi ameelezea wasiwasi wake mkubwa kwamba maafa yaweza kutokea kutokana na ukosefu wa huduma za afya, kwa sababu kambini, wakimbizi wengi wanasumbuliwa na ugonjwa wa Malaria, huku watoto wakisumbuliwa na ugonjwa wa kuharisha.

Idadi ya NGOs 130

Tangu tarehe Oktoba 1, serikali ya Burundi ilisitisha shughuli za NGOs 130 kwa kipindi cha miezi 3 kwa madai kuwa yanafanya kazi bila kuheshimu sheria za nchi.

Mashirika hayo yamepewa masharti ili yaruhusiwe tena kufanya kazi, moja ya masharti hayo ikiwa kuajiri wafanyakazi kwa kufwatisha usawa kati ya makabila muhimu ya Burundi na kusaini mkataba mpya na wizara ya fedha unao walazimisha mashirika hayo kuweka pesa zao zote za kigeni za matumzi kwenye benki kuu ya taifa.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Patrick Nduwimana, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG