Mkuu wa jeshi la Uganda, ambaye ni mtoto wa kiume wa rais Yoweri Museveni, Generali Muhoozi Kainerugaba, amesema kwamba hakuna rais atakayeongoza Uganda na kwamba hilo ni jukumu la wanajeshi au polisi.
Mahakama ya juu nchini Burundi Alhamisi ilithibitisha kifungo cha maisha dhidi ya waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Jenerali Alain Guillaume Bunyoni, chanzo cha mahakama kimeliambia shirika la habari la AFP.
Dunia leo inaadhimisha siku ya wakimbizi, kauli mbiu ikiwa ni “mshikamano na wakimbizi.”
Waziri mkuu wa Burundi aliyefutwa kazi Alain-Guillaume Bunyoni amefika mahakamani kukata rufaa dhidi ya hukumu yake kwa tuhuma zinazojumuisha kujaribu kupindua serikali, chanzo cha mahakama na mashahidi walisema Jumanne.
Rwanda siku ya Jumapili ilipuuzilia mbali madai ya Burundi kwamba iliwapa silaha kundi la waasi linaloshutumiwa kwa milipuko ya guruneti na kujeruhi watu kadhaa, na kuzidisha uhusiano mbaya kati ya majirani hao wa Afrika Mashariki.
Rais wa Kenya William Ruto ametangaza Ijumaa wiki hii kuwa siku kuu ya kitaifa kuomboleza vifo vya watu 238 waliofariki kutokana na mafuriko.
Mwaka huu Sherehe za Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi zina hisia ya dharura ya kujitolea upya kwa haki za kijamii, wakati tunapopitia kipindi kigumu, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko ya haraka katika sehemu za kazi kutokana na maendeleo ya teknolojia.
Mafuriko makubwa yameyakumba maeneo mengi ya Afrika Mashariki ambayo yanakabiliwa na mvua za mfululizo, Burundi ikiomba msaada wa kimataifa wa kuisaidia kupambana na maafa hayo.
Serikali ya Burundi na Umoja wa Mataifa wameanzisha mchakato wa kuomba msaada wa ufadhili wa fedha ili kukabiliana na athari mbaya za mvua kubwa zinazonyesha kwa miezi kadhaa ambazo zimewakosesha makazi takriban watu 100,000.
Poland ilisema Jumapili kwamba itaitaka Russia kueleza ukiukaji mpya wa anga baada ya kombora la Russia kuingia kwenye anga ya nchi hiyo ya NATO kwa takriban kilomita 2 Jumapili asubuhi kabla ya kurejea Ukraine, kulingana na msemaji wa jeshi la Poland.
Chama kikuu cha upinzani nchini Burundi kilikumbwa na mgawanyiko Jumapili baada ya tawi lake kusema kuwa limemuondoa kiongozi wa chama hicho Agathon Rwasa kwa kushindwa kuunganisha pande mbili zinazolumbana.
Serikali ya Haiti iliomba rasmi msaada wa usalama kutoka kwa nchi zote kote duniani, zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Pandisha zaidi