Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:42

Waziri mkuu wa Burundi aliyefutwa kazi akata rufaa dhidi ya hukumu yake


Alain-Guillaume Bunyoni (kulia) akizungumza na afisa wa polisi huko Bunjumbura Aprili 12 2016, wakati alipokuwa Waziri wa Usalama wa Burundi. Picha na STRINGER / cds / AFP.
Alain-Guillaume Bunyoni (kulia) akizungumza na afisa wa polisi huko Bunjumbura Aprili 12 2016, wakati alipokuwa Waziri wa Usalama wa Burundi. Picha na STRINGER / cds / AFP.

Waziri mkuu wa Burundi aliyefutwa kazi Alain-Guillaume Bunyoni amefika mahakamani kukata rufaa dhidi ya hukumu yake kwa tuhuma zinazojumuisha kujaribu kupindua serikali, chanzo cha mahakama na mashahidi walisema Jumanne.

Akiwa mmoja wa waliokuwa vigogo wenye nguvu serikalini, Bunyoni alikuwa waziri mkuu kutoka katikati ya mwaka 2020 hadi Septemba 2022 alipofutwa kazi, siku chache baada ya Rais Evariste Ndayishimiye kuonya kuhusu madai ya njama za mapinduzi dhidi yake.

Alihukumiwa mwezi Desemba kifungo cha maisha jela kwa msururu wa mashtaka yakiwemo kupanga njama ya kupindua utawala wa kikatiba pamoja na kutumia uchawi kutishia maisha ya rais, kudhoofisha usalama wa taifa, kuyumbisha uchumi na kujitajirisha kinyume cha sheria.
Jenerali huyo wa jeshi, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 52, alikuwa amekana mashtaka yote na kusema anapaswa kuachiliwa kwa sababu ya ukosefu wa ushahidi.

Forum

XS
SM
MD
LG