Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:44

Kenya kuomboleza vifo kutokana na mafuriko kwa kupanda miti


Uharibifu uliosababishwa na mafuriko katika kijiji cha Kamuchiri, Mai Mahiu, Kenya April 30 2024
Uharibifu uliosababishwa na mafuriko katika kijiji cha Kamuchiri, Mai Mahiu, Kenya April 30 2024

Rais wa Kenya William Ruto ametangaza Ijumaa wiki hii kuwa siku kuu ya kitaifa kuomboleza vifo vya watu 238 waliofariki kutokana na mafuriko.

Ruto amesema maombolezi yatafanyika kwa kupanda miti ili kusaidia katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kenya, pamoja na nchi nyingine za Afrika Mashariki, zimekabiliwa na mafuriko ambayo yamepelekea zaidi ya watu 235,000 kuachwa bila makao na darzeni wanaishi katika kambi.

Rais Ruto vile vile ametangaza kufunguliwa kwa shule kote nchini, baada ya masomo kuahirishwa kwa wiki mbili kutokana na mvua kubwa na baadhi ya shule kuharibiwa na mafuriko.

Serikali ya Kenya imesema kwamba zaidi ya shule 1,000 zimeathiriwa kutokana na mafuriko hayo na pesa zimebajetiwa kwa ukarabati.

Watabiri wa hali ya hewa nchini Kenya wanasema kwamba mvua kiasi itaendelea kunyesha katika siku zijazo, katika sehemu kadhaa za nchi.

Forum

XS
SM
MD
LG