Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:30

Rwanda yapuuzilia mbali madai ya Burundi kwamba iliwapa silaha kundi la waasi

Rais wa Rwanda Paul Kagame akiongea na watu waliokimbia makazi yao kutokana na mafuriko katika kambi ya wakimbizi ya Inyemeramihigo huko Rubavu Mei 12, 2023. Picha na Mariam KONE / AFP
Rais wa Rwanda Paul Kagame akiongea na watu waliokimbia makazi yao kutokana na mafuriko katika kambi ya wakimbizi ya Inyemeramihigo huko Rubavu Mei 12, 2023. Picha na Mariam KONE / AFP

Rwanda siku ya Jumapili ilipuuzilia mbali madai ya Burundi kwamba iliwapa silaha kundi la waasi linaloshutumiwa kwa milipuko ya guruneti na kujeruhi watu kadhaa, na kuzidisha uhusiano mbaya kati ya majirani hao wa Afrika Mashariki.

Takriban watu 38 walijeruhiwa katika shambulio la siku ya Ijumaa mjini Bujumbura, wizara ya mambo ya ndani ya Burundi ilisema, ikitoa lawama kwa waasi wa RED-Tabara.

Gitega alisema Kigali ilitoa mafunzo na msaada wa vifaa kwa waasi, ambao wamekuwa wakipigana na serikali ya Burundi kutoka katika kambi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo alikanusha madai hayo, akisema hayana uhusiano kabisa na shambulio hilo.

Burundi ina tatizo na Rwanda, lakini hatuna tatizo na Burundi, ofisi yake ilisema katika taarifa yake.

Tunatoa wito kwa Burundi kutatua matatizo yake ya ndani na kutoihusisha Rwanda na mambo hayo mabaya.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili mara nyingi umekuwa wenye matatizo na Rwanda hapo awali ilikanusha madai ya kuwa inaunga mkono waasi.

Forum

XS
SM
MD
LG