Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:53

Uganda yaanza kutoza ushuru mitandao ya jamii


Mitandao mbalimbali ya jamii duniani
Mitandao mbalimbali ya jamii duniani

Uganda imekuwa nchi ya kwanza duniani kuanza kutoza ushuru wa matumizi ya mitandao ya kijamii Jumapili lengo likiwa kupata pesa za kutosha kugharamia uimarishaji wa miundombinu sekta za umma.

Serikali pia inawatoza ushuru wanaoweka akiba ya pesa kwa simu zao za mkononi, kutuma au kupokea pesa kupitia.

Ni hatua inayo onekana kuwakera wana harakati wa kijamii na wanaotumia mitandao ya kijamii ya whatsapp, facebook, you tune, twitter, skype, Instagram, miongoni mwa nyingine.

Kila siku, anayefungua tu mitandao ya kijamii, atalipia shilingi Mia mbili, hatua ambayo itaiwezesha serikali kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 34 kila siku.

Kwa wanaoweka pesa zao kwa simu kama akiba, wanatozwa shilingi 500 bila kuzingatia kiwango, kila wanapotuma pesa, na anayepokea vile vile hutozwa kiwango hicho.

Serikali inasisitiza kwamba lazima ada hizo zilipiwe, huku rais Museveni akisema kwamba hatua hiyo inalenga kudhibiti uenezaji wa kile alichokitaja kama porojo kwenye mitandao.

Lakini wanaotumia mitandao ya kijamii, wanasema kwamba hawatalipa ushuru huo, na wengi wamepakua programu ya VPN inayomwezesha anayetumia mitandao ya kijamii kutogunduliwa au kunaswa na mitambo ya serikali.

Wengine wameamua kutumia mtandao wa WI-FI, huku wengine wakitumia nambari za simu kutoka nchi jirani kama Safaricom ya Kenya.

Kulingana na taarifa ya mamlaka ya kutoza ushuru nchini Uganda URA, kati ya mitandao ya kijamii inayotozwa ushuru 61, ni mtandao wa Grindr, unaotumika na watu walio katika uhusiano wa kimapenzi wa jinsia moja, wakati tendo hilo ni kinyume cha sheria nchini Uganda.

Taarifa ya pamoja ya kampuni kubwa tatu za mawasiliano nchini Uganda MTN, Bharti Airtel na Africell, inaarifu kwamba kampuni hizo zina wajibu wa kutekeleza sheria, zikifutilia mbali matangazo yote ya punguzo kwa wale wanaotumia internet.

Kulingana na mtandao wa kundi linalotetea maswala ya digital, digital advocacy group, gharama ya data barani Afrika ni miongoni ama gharama juu zaidi duniani.

Hatua ya Uganda kutoza ushuru mitandao ya kijamii, inahofiwa kwamba itaongeza gharama hizo.

Takwimu ambazo zimechapiswa na mamlaka ya mawasiliano nchini Uganda, UCC, zinaonyesha kwamba Uganda ina idadi ya watu millioni 41. 24 kati yao wanamiliki simu huku watu milioni 17 wakiwa wanatumia mitandao ya kijamii.

Wakosoaji wa serikali wanasema kwamba ushuru kwa mitandao ya kijamii unalenga kuminya uhuru wa kujieleza na kusambaza habari.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kennes Bwire, Washington, DC

XS
SM
MD
LG