Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:06

Mabalozi nchini Tanzania wahoji katazo dhidi ya gazeti The Citizen


Rais John Pombe Magufuli
Rais John Pombe Magufuli

Wanadiplomasia nchini Tanzania kutoka nchi nane za Umoja wa Ulaya, Ijumaa, wamehoji uamuzi wa kusitishwa kwa muda wa wiki moja chapisho la gazeti la Kiingereza baada ya maafisa wa serikali ya Tanzania kulishutumu limepotosha suala la bei ya kubadilisha fedha za kigeni.

Gazeti la The East African limeripoti kuwa hatua hiyo iliyochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya gazeti la 'The Citizen' imekuja wakati malalamiko kwa upande wa wanaounga mkono upinzani na makundi ya taasisi za kiraia yanaongezeka kwa kile wanachosema kuwa ni hatua ya serikali kuua upinzani na kuweka vikwazo kwa waandishi wa habari na wapiganiaji wa haki za binadamu.

Kauli ya mabalozi nchini Tanzania

“Kwa kawaida, naanza siku yangu kwa kusoma baadhi ya magazeti, likiwemo gazeti lililofungiwa la The Citizen, “Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Sarah Cooke ameandika katika akaunti yake ya Twitter.

“Hilo sio sawa, limefungiwa nchini Tanzania kwa siku saba. Je, adhabu inalingana na kosa linalodaiwa kufanyika?’

Ujumbe kama huo pia ulikuwa umepostiwa na mabalozi wa Belgium, Denmark, Ujermani, Ireland, Italy, Uholanzi na Sweden, katika kitendo ambacho ni nadra cha kupinga waziwazi kwa pamoja hatua hiyo ya serikali.

“Vyombo vya habari vinajukumu muhimu katika kuanzisha mijadala ya umma,” Ubalozi wa Ireland uliandika, na kusema imesikitishwa na uamuzi wa wiki hii kusitisha kwa muda chapisho la The Citizen.”

Gazeti la Citizen lilikuwa limeshutumiwa kwa kutoa habari za upotoshaji katika habari iliyochapishwa hivi karibuni juu ya kushuka thamani kwa shilingi ya Tanzania.

Liliripoti kuwa dola ya Marekani ilikuwa inanuliwa kwa thamani ya Tsh 2,415 ukilinganisha na ile ya Benki Kuu ya Tanzania ya 2,300, kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa katika maduka ya kubadilisha sarafu za kigeni na mabenki.

Sheria ya Takwimu ya 2017 inapiga marufuku uchapishaji wa habari zozote zinazohusu takwimu zinazopingana na takwimu za serikali, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa wale waliochapishwa habari hizo kufungwa jela.

Wanaomkosoa Magufuli

Rais John Magufuli anakabiliwa na ukosoaji unaoendelea kuongezeka kutoka vyama vya upinzani pamoja na makundi ya taasisi za kiraia na jumuiya ya kimataifa kwa kile wanachosema ni ukandamizaji wa haki za binadamu.

Kundi la Media rights group, ambao ni waandishi bila ya mipaka, wamesema kuwa kusitishwa kwa muda huko kwa 'The Citizen' “ni kielelezo tosha cha kuendelea kushuka kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania tangu Rais John Magufuli achukuwe madaraka.”

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), taasisi kuu ya haki za binadamu nchini Tanzania, kimesema kusitishwa huko kwa gazeti hilo ni “ muendelezo wa kukandamiza uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania.”

XS
SM
MD
LG