Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:39

Magufuli awaonya wapinzani, asema wasipo ‘heshimu sheria’ wataishia jela


Rais John Pombe Magufuli
Rais John Pombe Magufuli

Rais John Magufuli amepeleka ujumbe wa Tanzania mpya kwa vyama vya upinzani nchini akiwaonya kuwa iwapo ‘hawataheshimu sheria’ wataishia jela.

Rais huyo amempa ujumbe huo waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye sasa ni kiongozi wa chama cha upinzani cha Chadema.

Magufuli ameongeza: "Hii ndio Tanzania mpya tunayoitaka..., "Nimeona hili nilizungumze kwa heshima kubwa, Mzee Lowassa, ili wale unaowaongoza kule, uende ukawashauri.

Katika ujumbe huo amesema:“otherwise (lasivyo) wataishia kwenye magereza ili wakajifunze namna ya kuheshimu sheria za Watanzania."

Tayari viongozi kadhaa wa upinzani Tanzania wakiwemo wa chama cha Chadema ambacho Lowassa ni mjumbe wa kamati kuu wanashtakiwa kwa tuhuma za uchochezi, na wengine kwa kutoa maneno yasiyofaa dhidi ya rais na wengine kwa kufanya mikusanyiko bila ya kibali.

Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alifutiwa dhamana pamoja na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana katika kesi inayowakabili ya kufanya mikusanyiko kinyume cha sheria.

Magufuli na Lowassa walikutana Jumanne Novemba 27 katika ufunguzi wa maktaba ya kisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

"Ninakupongeza sana (Lowassa). Hii ndiyo Tanzania mpya tunayoitaka. Vyama vyetu visiwe chanzo cha kututenganisha, bali viwe chachu ya kuleta maendeleo," amesema Rais.

Magufuli amemsifia Lowassa kuwa pamoja na kumshinda kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, ameendelea kuwa mtulivu.

XS
SM
MD
LG