Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:03

Barua ya Wazi : CPJ yamtaka Magufuli kuchukua hatua


Angela Quintal, Kulia, na Muthoki Mumo,
Angela Quintal, Kulia, na Muthoki Mumo,

Kamati Maalumu ya Kuwalinda Wanahabari Duniani (CPJ) imemwandikia barua Rais wa Tanzania John Magufuli kueleza kushtushwa kwao na vitendo walivyofanyiwa wafanyakazi wa timu yake ya programu ya Afrika ambao walikamtwa na kuwekwa kizuizini na maafisa wa Tanzania Novemba 7.

"Ni matarajio yetu kuwa, kama sisi, tumeumizwa na vitendo hivi ambavyo ni kinyume cha weledi wa kikazi; tabia ya unyanyasaji, na wewe utaweza kuagiza uchunguzi ufanyike na kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na hili," CPJ imeeleza.

"Pia tumeshutshwa sana kwa taarifa kuwa waandishi waliokuwa wamekutana na timu yetu wamekuwa wakikabiliwa na shinikizo kubwa na vitisho. Tunakuhimiza kuhakikisha kuwa waandishi wa Tanzania hawalengwi kwa sababu ya kazi yao," imeongeza.

CPJ inamtaka Magufuli kuwajulisha juu ya jawabu la serikali yake juu ya hili. "Tutakuwa tunafuatilia kupitia wawakilishi wa ubalozi wa nchi yako, imehitimisha barua hiyo."

Barua hiyo ilioandikwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CPJ, Joel Simon, imeeleza kuwa Angela Quintal, anaye ongoza programu ya CPJ Afrika na Muthoki Mumo, mwakilishi wa CPJ katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara, walisafiri kwenda Tanzania Octoba 31 wakiwa na nia ya kuendelea na ziara yao mpaka Novemba 10.

Ameandika kuwa Lengo la wafanyakazi hao ilikuwa ni kuwatembelea waandishi wa habari wa Tanzania na taasisi za jumuiya za kiraia ili kupata uelewa zaidi juu ya uhuru wa habari katika nchi yako rais.

Kadhalika walikuwa wamealikwa na Baraza la Habari la Tanzania (MCT). Kabla ya kusafiri kuja Tanzania, walizungumza na wawakilishi wa serikali yako ambao waliwafahamisaha kuwa visa zilikuwa hazihitajiki kwa kuwa walikuwa wamepanga kufanya mikutano binafsi.

Mkurugenzi Mtendaji huyo ameeleza kuwa Quintal, raia wa Afrika Kusini, na Mumo, Mkenya walikuwa wameeleza nia yao wakiwa katika forodha ya Dar es Salaam, waliruhusiwa kuingia bila tatizo lolote, na walikuwa wakifanya shughuli zao waziwazi. Kwa bahati mbaya ziara yao ilisitishwa ghafla na maafisa waliowakabili kutoka serikali yako.

Jioni ya Novemba 7, maafisa wa serikali wakiwa katika nguo za kiraia ambao walijitambulisha kuwa ni maafisa wa uhamiaji walifika na kuingia ndani ya vyumba vya Quintal na Mumo hotelini, wakapekuwa vitu vyao na kuwalazimisha kuwa lazima waende wakahojiwe.

"Timu hiyo ya CPJ ilipandishwa kwenye gari kwa mabavu na madirisha kuwa yamefunikwa, na kupelekwa katika eneo lisilojulikana na wakawa wanahojiwa," CPJ imesema.

Quintal na Mumo hawakuhojiwa lolote kuhusu visa zao. Kinyume chake, maafisa hao walidai walikuwa wanafuatilia timu yetu kwa masiku na wakawa wanawauliza maswali hayo kwa hayo juu ya maudhui ya mikutano yao, imesema barua hiyo.

Imeongeza kuwa maafisa hao walikuwa wamemdhamiria Mumo na kutumia utesaji wa kimwili na kisaikolojia. Walimpiga vibao na kumsukuma. Walimtuhumu kuwa anawasaliti watu weusi. Walimtishia kutumia utesaji zaidi. Moja wa hao maafisa alisema ingekuwa ni amri yake, angewauwa.

Maafisa hao pia walikamata pasi za kusafiria za timu hiyo ya CPJ na vifaa vyao vya kielektronikia, na kumlazimisha Quintal na Mumo kuwapa neno la siri la vifaa vyao vya kieletronikia ili wale maafisa waweza kujaribu kuingia kudukuwa taarifa zao, barua hiyo imeeleza.

Barua hiyo inaeleza pia wakati wote huo wako kizuizini, maafisa hao waliweza kuingia kwenye akaunti yake Quintal binafsi ya Twitter na kutuma ujumbe wa uongo wakidai kuwa timu hiyo ya CPJ ilikuwa imeachiwa.

"Tunatambua kuwa serikali yako, kama serikali zote, zina amri ya kisheria kuzuia watu kuingia nchini mwako na kudhibiti visa.Lakini, kuwekwa kizuizini kwa Quintal na Mumo, kuna kitu ambacho ni cha msingi zaidi, nacho ni utayari wa serikali yako kuendeleza uhuru wa habari na kuruhusu taasisi za kimataifa kama vile CPJ kuweza kuingia nchini na kufanya tathmini yake bila ya kuingiliwa na mtu yoyote," imeainisha barua hiyo.

CPJ imeeleza kuwa : "Iwapo Quintal na Mumo walikuwa wamepewa taarifa zenye makosa juu ya visa na wawakilishi wa serikali yako, wangeweza kukataliwa kuingia nchini au kurejeshwa.

"Kwa kweli hakuna njia yoyote ya kuhalalisha namna walivyotendewa wakiwa katika mikono ya maafisa wa serikali ya Tanzania, ambao tunaamini walikuwa siyo maafisa wa uhamiaji, bali ni wafanyakazi wa usalama wa taifa," imesisitiza barua hiyo.

"Lakini hii dosari inaweza kurekebishwa iwapo serikali yako itachukuwa hatua zipasazo kwa haraka.Tunaomba utuhakikishie kuwa ujumbe wa CPJ utaruhusiwa kutembelea Tanzania katika siku za karibuni; kwamba ujumbe wa wanachama wa CPJ upatiwe visa stahili bila ya kuchelewa; na waruhusiwe kufanya kazi yao bila ya kuingiliwa; na kwamba waandishi wa Tanzania wakutane na ujumbe huo bila ya kuogopa kulipiziwa kisasi."

CPJ imesema : Sifa ya Tanzania kama nchi ni ya kuheshimu uhuru wa habari na wageni wa kimataifa na ni yenye kusimamia majukumu yake kama mwanachama wa jumuiya ya kimataifa imeingia doa kwa kuwatendea ubaya timu ya CPJ.

XS
SM
MD
LG