Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:10

Afrika : Waandishi waeleza serikali kandamizi zinavyo wanyanyasa


Waandishi wa CPJ Angela Quintal (Kulia) ambaye ni raia wa Afrika Kusini na Mumo Muthoki (kushoto), raia wa Kenya waliokamatwa nchini Tanzania, serikali ikidai kuwa waliingia nchini na kufanya shughuli zao kinyume na kibali cha matembezi walichokuwa wamepewa.
Waandishi wa CPJ Angela Quintal (Kulia) ambaye ni raia wa Afrika Kusini na Mumo Muthoki (kushoto), raia wa Kenya waliokamatwa nchini Tanzania, serikali ikidai kuwa waliingia nchini na kufanya shughuli zao kinyume na kibali cha matembezi walichokuwa wamepewa.

Kuwa mwandishi wa habari za uchunguzi barani Afrika- ambako viongozi na baadhi ya serikali zimekuwa zikijulikana kuwa zinawatishia waandishi wa habari na kuwakamata, kuwateka na hata kuwauwa- na hivyo imekuwa inawawia vigumu waandishi hao kufanya kazi yao kwa urahisi.

Lakini waandishi wanatatizwa katika sehemu mbalimbali barani Afrika na wanasema wana wasiwasi juu ya tishio kwa waandishi nje ya mipaka yao: kauli za uadui za viongozi wa dunia, wanasema, zinatishia kazi zao muhimu, Sauti ya Amerika inaripoti.

Kuna vitisho vinavyotolewa na watu wasiojulikana, bughudha za mapolisi, maafisa wa serikali wenye vitendo vya ukatili. Kadhalika kumekuwepo muendelezo wa wingu lililotanda la kujizuia kuandika baadhi ya mambo, kutengwa kijamii na kulazimishwa kuishi uhamishoni (ukimbizini) na juu ya yote hayo yanayowakabili waandishi ni kipato cha chini kabisa.

CPJ yaitaja Tanzania

Nchini Tanzania, Kamati Maalumu ya Kuwalinda Wanahabari Duniani (CPJ) inasema kuwa serikali kwa kipindi cha miaka mitatu imekuwa ikitekeleza sheria kandamizi na kuwabughudhi waandishi wa habari na blogi.

Mwandishi Kelvin Matandiko anasema anahisi hali hiyo kila siku.

Anasema : “Inashitua kwa waandishi wengi ambao walikuwa wamezoea kufanya kazi katika mazingira huru kama Tanzania. Lakini hali ilivyo hivi sasa ya utawala wa siasa ambao umeingia madarakani na mabadiliko mapya na hatujui nini kilicho sababisha hali hii, lakini tunaamini hili linafanyika kuuwa sekta ya uandishi wa habari."

Uhalisia wa uandishi wa uchunguzi

Mwandishi wa VOA anaripoti kuwa Ili kuweza kufahamu uhalisia wa maisha ya mwandishi wa habari za uchunguzi katika bara la Afrika, kuna simulizi za ukandamizaji, mauaji na kubughudhiwa, kufungwa zinazowakabili kitu ambacho kinafanya maisha yao yawe magumu.

Anton Harber, Profesa wa Uandishi Afrika Kusini na muandaaji wa mkutano wa kila mwaka unaowaleta mamia ya waandishi wa habari za uchunguzi wa Afrika mjini Johannesburg kila mwaka, huwezesha waandishi kuzungumza kwa kubadilishana mawazo na kutengeneza mawasiliano.

Uandishi na Ufisadi

Waandishi wa habari hapa wameweza kuibua vitendo vya ufisadi, uvunjifu wa haki za binadamu, makundi ya kivita, madawa ya kulevya na uhalifu wa wanyama pori, na matendo mengine yasiokubalika kisheria.

Pamoja na kuwepo makundi ya wahalifu hawa sugu, Muno Gedi anastahili sifa. Yeye ni mwandishi wa habari za uchunguzi kwa kile kinawezekana kuwa ni moja ya maeneo magumu duniani : mji mkuu wa Somalia.

Anaandika vitu kama vile utamaduni wa kuwatairi wanawake, kuuzwa kwa chakula cha misaada kinachotolewa na mashirika ya kimataifa katika kambi za wakimbizi na hali inayoendelea ya vita kati ya koo za Kisomali na makundi ya wapiganaji.

Vitisho vya watu wasiojulikana

Gedi anasema mara nyingi anapokea vitisho, vingi vikitokana na watu wasio julikana.

“Nafikiri uandishi wa habari za uchunguzi katika dunia siku zote ni jambo hatarishi, hususan Somalia, ni eneo lenye hatari. Kwa hivyo ukifanya kazi kama hii Somalia, siyo jambo rahisi.”

Nchi hatari kuliko zote

Anasema kwa uchache : Waandishi bila ya mipaka wanasema Somalia ni nchi hatari kuliko zote kwa waandishi nchi za kusini mwa jangwa la sahara - Afrika, na mwaka 2018 waandishi wawili wameuwawa.

Haya yote mchapishaji Dapo Olorunyomi hatima yake ni ukweli. Na katika nchi yenye sifa mbaya ya ufisadi, Nigeria, anasema wakati mwengine inamaanisha kueleza hatari ambazo zinatokana na uandishi wenyewe.

Waandishi wa VOA

Ameainisha kufukuzwa kazi hivi karibuni kwa waandishi 15 wa Idhaa ya Hausa- VOA baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa walipokea malipo yasiyo kubalika kutoka kwa afisa wa ngazi ya juu.

Anasema kuwa kile kinachofanya uandishi wa uchunguzi kuwa mgumu: ukweli huwa juu ya kila kitu, hata pale unapokuwa ukweli huo unaumiza.

XS
SM
MD
LG