Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:10

Somaliland yakamata waandishi, kufungia vituo vya televisheni


Ramani ya Somaliland na Puntland
Ramani ya Somaliland na Puntland

Serikali katika eneo lililojitangazia mamlaka ya kujitawala la Somaliland imetakiwa kuacha kuwazuilia na kuwanyanyasa waandishi wa habari wanaoripoti mgogoro uliopo kati yake na Puntland na kuondoa katazo lililowekwa dhidi ya stesheni za televisheni mbili, Kamati ya Kuwalinda Waandishi (CPJ) imesema Ijumaa.

Waandishi wa habari wawili, Abdirahman Keyse Mohamed, ambaye anajulikana kama Tungub, na Mohamed Ahmed Jama, ambaye anajulikana kama Bidhaanshe, walikamatwa.

Tungub alikamatwa Mei 27 na Bidhaanshe alikamatwa Mei 28, wote wakiwa katika mji wa Las Anod katika Mkoa wa Sool uliokuwa na mgogoro, kwa mujibu wa kauli ya mkurugenzi mtendaji wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Somaliland na Guleid Ahmed Jama, mwenyekiti wa taasisi ya utetezi katika kituo cha haki za binadam.

Abdirahman ameiambia CPJ kuwa yeye na Mohamed walizuiliwa katika kituo cha polisi huko Las Anod hadi Mei 30, ambapo walipelekwa kwenye kituo kikuu cha mahabusu cha mji huo.

Hakuna kati yao aliyefunguliwa mashtaka na wala hawakufikishwa mahakamani, na jana walipewa dhamana na kuachiwa, Abdirahman aliwa CPJ.

Jambo hili linakiuka kifungu cha 27 cha katiba ya Somaliland, ambacho kinataka kila mtu anayekamatwa kupelekwa mahakamani katika kipindi cha saa 48.

Abdirahman, mwandishi anayefanya kazi na kituo binafsi kinachomiliki Televisheni ya Bulsho, ameiambia CPJ kuwa vyombo vya usalama katika eneo hilo havikumfahamisha ni kwa nini walimkamata.

Katika habari aliyoripoti Mei 26, alikuwa amewahoji wananchi juu ya mgogoro uliopo kati ya Puntland na Somaliland, Abdirahman, Yahye, na naibu meneja wa Televisheni ya Bulsho, Abdirashid Nour Wais, wameiambia CPJ.

Asubuhi Mei 28, polisi walimzuilia Abdirahman na waandishi wengine kuripoti mkutano wa serikali za mitaa uliokuwa unazungumzia mgogoro kati ya mikoa hiyo miwili.

Abdirahman amesema maafisa hao pia walivunja kamera yake. Baadae alikamatwa siku hiyo asubuhi akiwa katika ofisi za Televisheni ya Bulsho huko Las Anod, aliiambia CPJ.

Naye Mohamed, Mwanadishi mmoja anayefanya kazi na kituo binafsi cha Televisheni cha SBS, ameiambia CPJ kuwa alikamatwa alipokuwa anaripoti maandamano huko Las Anod.

Mnamo Mei 29, wizara ya habari Somaliland ilikifungia kituo cha TV cha SBS na kituo kingine binafsi, SOMNews, ikivitaka visiendelee na matangazo yao Somaliland, kwa mujibu wa maelezo ya Guleid, Yahye na tamko lililotolewa na serikali.

Wizara ya Habari ilivituhumu vituo hivyo kwa kutoa habari zisizo sahihi na kueneza “shambulizi la propaganda” dhidi ya Somaliland, kwa mujibu wa tamko la serikali na tamko lililotolewa na Kituo cha Haki za Binadamu.

Wizara iliamrisha polisi kufunga matawi yote ya vituo vya habari vya SOMNews na SBS katika Somaliland na kutishia wale wanaopeleka habari kwenye vituo hivyo viwili kuwachukulia hatua za kisheria, kwa mujibu wa tamko la serikali.

Pamoja na shughuli za ukusanyaji wa habari kupigwa marufuku Somaliland, watazamaji wa vituo vya televisheni katika eneo la Somaliland waliendelea kupata matangazo kupitia maudhui ya satellite yanayorushwa na vituo hivyo viwili jana mchana, kwa mujibu wa maelezo ya Guleid.

XS
SM
MD
LG