Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:17

Jeshi la Somalia limewauwa al-shabaab 13


Wanajeshi wa Somalia wakihudhuria katika mafunzo yaliokuwa yanaendeshwa na Jeshi la Uturuki, Mogadishu, Somalia, Septemba 30, 2017.
Wanajeshi wa Somalia wakihudhuria katika mafunzo yaliokuwa yanaendeshwa na Jeshi la Uturuki, Mogadishu, Somalia, Septemba 30, 2017.

Mapambano kati ya majeshi ya Somalia yakiwasaidia wanakijiji na wapiganaji wa al-Shabaab yameuwa sio chini ya wapiganaji 13, mashuhuda na maafisa wamesema.

Mapambano kati ya majeshi ya Somalia yakiwasaidia wanakijiji wa eneo hilo na wapiganaji wa al-Shabaab yameuwa sio chini ya wapiganaji 13, mashuhuda na maafisa wamesema.

Mapambano hayo yaliyotokea katikati ya nchi ya Somalia Jumamosi yalianza baada ya wapiganaji wa al-Shabab wenye silaha walipojaribu kuwatoza kodi wakazi wa Halfoley, kijiji kilichopo karibu na mji wa Jalalaqsi, katika mkoa wa Hiran.

Abdi Dahir Guure, mkuu wa wilaya wa mji wa Bulabarde wa mkoa huo, ameiambia VOA kuwa wanajeshi wa serikali, wakiwasaidia wachugaji ngombe, walipambana kwa zaidi ya masaa matano katika mapambano makali dhidi ya wapiganaji hao.

"Mapambano hayo yalitokea majira ya saa moja asubuhi wakati wapiganaji wenye silaha nzito walipowashambulia wanavijiji baada ya kukataa shinikizo lao wakiwalazimisha watoe baadhi ya mifugo yao kama malipo ya Zaka au ushuru," amesema Guure.

"Majeshi ya serikali, yalipelekwa ili kuwalinda wafugaji, na mara moja yakaingia katika mapambano, na kuwauwa wapiganaji wasiopungua 13.

Maafisa wa serikali ya Somalia katika mkoa huo wamesena vukosi vingine vya jeshi la taifa la Somalia vilikuwa vimesogea katika vijiji vingine katika mkoa huo ili kuwazuia wapiganaji wasiweze kujikusanya tena na kurejesha mashambulizi dhidi ya wafugaji.

Mashuhuda mbalimbali binafsi waliwasiliana na VOA kuthibitisha kile serikali ilitangaza, wakisema walishuhudia miili takriban 13 ya wapiganaji hao. Wafugaji wawili pia walijeruhiwa wakati wa mapambano hayo.

XS
SM
MD
LG