Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:01

Wabunge Kenya wawatishia waandishi kwa kuripoti madai ya ufisadi


Nakala ya ripoti ya CPJ kuhusu hali ya uhuru wa habari nchini Kenya iliotolewa Julai 15, 2015.
Nakala ya ripoti ya CPJ kuhusu hali ya uhuru wa habari nchini Kenya iliotolewa Julai 15, 2015.

Wabunge wa Kenya wametakiwa kuacha kuwanyanyasa waandishi na kuwaruhusu kuripoti masuala ya bunge bila ya kuogopa visasi, shirika la kimataifa la kuwalinda waandishi CPJ imesema Ijumaa.

Dinah Ondari na Anthony Mwangi, waandishi wa habari wanaofanya kazi na gazeti la Kenya People Daily, wiki hii walikosolewa wakati wa kikao cha bunge, wakitishiwa kuwa watazuiliwa kuripoti kuhusu bunge, na kuitwa na kamati ya bunge, kwa mujibu wa rikodi za bunge, Hansard ya Julai 31, inayoweka kumbukumbu ya mazungumzo yote yanayofanyika bungeni. Pia hilo lilielekezwa kwa Ken Bosire, mkurugenzi mkuu wa gazeti hilo.

Tukio hili linatokana na kuchapishwa katika gazeti la People Daily Julai 30 na 31 habari zinazodai kuwa wabunge walikuwa wanachukuwa na kuomba rushwa kutoka katika taasisi na watu mbalimbali ambao walikuwa wanatakiwa kuwachunguza. Gazeti la People Dailiy linamilikiwa na mtu binafsi, lakini linahusishwa kuwa na mafungamano na familia ya Rais Uhuru Kenyatta.

“Iwapo wabunge wa Kenya wanania ya kupambana na ufisadi, jaribio la kuwatishia waandishi kwa ajili ya kuwanyamazisha ni lazima liachwe mara moja,” amesema Mwakilishi wa CPJ kusini mwa jangwa la sahara Afrika Muthoki Mumo.

“Tunawahimiza wabunge kuacha kujaribu kuwatishia Dinah Ondari, Anthony Mwangi, na wafanyakazi wenzao kwa kutumia vitisho na kuwachunguza na badala yake wawaachie huru kufanya kazi yao ya kuripoti bungeni.

Mnamo Julai 31 katika Bunge la Taifa, moja kati ya mabunge mawili, Mbunge Robert Pukose, mbunge wa chama tawala cha Jubilee, alilishutumu gazeti la People Daily kwa kosa la “kulitukana” bunge na kusema kuwa ripoti yake ilikuwa ya kulaani kwa jumla wabunge wote, kwa mujibu wa ripoti ya Hansard.

Kwa mujibu wa ripoti ya Hansard, Pukose alimtaka spika wa Bunge la Taifa, Justin Muturi, “kuchukua hatua” dhidi ya gazeti la People Daily na kuamuru kamati ya bunge kuanzisha uchunguzi dhidi ya gazeti hilo kutokana na ripoti zao.

Kauli ya Pukose iliungwa mkono na wabunge wengine akiwemo Kiongozi wa walio wengi bungeni Aden Duale na kiongozi wa walio wachache John Mbadi, kwa mujibu wa Hansard.

Kwa kujibu ombi la wabunge, Muturi alichukua hatua ya kuitaka kamati ya bunge kuchunguza madai hayo, kwa mujibu wa Hansard.

Hata hivyo Muturi alisema kuwa hakuna uamuzi ambao utafanyika kuwazuia waandishi au vyombo vya habari “mpaka pale kamati hiyo itakapotoa mapendekezo yake kwa njia moja au nyingine,” kwa mujibu wa Hansard.

XS
SM
MD
LG