Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:14

Mnangagwa aamrisha kufukuzwa kwa waandishi kuchunguzwe


Nelson Chamisa
Nelson Chamisa

Rais mteule wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, amekemea vikali uamuzi wa polisi Ijumaa, kuwafukuza waandishi wa habari waliokuwa wamejitokeza kukutana na mgombea wa upinzani Nelson Chamisa.

Waandishi wa habari walikuwa wanamsubiri kiongozi wa upinzani wa chama cha MDC Nelson Chamisa ili waweze kuzungumza nao juu ya uamuzi wake wa kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais.

Katika ujumbe wa tweeter, Rais Mnangagwa anasema tukio hilo lilitokea katika hoteli ya Bronte halikubaliki kabisa katika jamii yao na kutaka uchunguzi wa kina ufanyike.

Aliongeza kusema haki ya kujieleza ni mojawapo ya misingi ya haki za binadamu inayo heshimiwa nchini humo na kila mtu ana haki ya kujieleza kwa njia huru.

Mapema Ijumaa, tume ya uchaguzi ya Zimbabwe ilimtangaza Mnangagwa kuwa mashindi, wa uchaguzi huo ulofanyika jumatatu akipata asili mia 50.8 ya kura, huku mpinzani wake wa karibu, Nelson Chamisa, akipata asili mia 44.3.

Chamisa mwenye umri wa miaka 40 anasema matokeo yamechakachuliwa na ameahidi kuwasilisha mashtaka mbele ya mahakama, akidai tena kwamba yeye ndiyer mshindi wa uchaguzi huo.

XS
SM
MD
LG