Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:53

Upinzani wakilaumu chama cha ZANU-PF


Watu wakiangalia baadhi ya matokeo ya uchaguzi nje ya ofisi za kupiga kura mjini Harare, Zimbabwe, Julai 31, 2018.
Watu wakiangalia baadhi ya matokeo ya uchaguzi nje ya ofisi za kupiga kura mjini Harare, Zimbabwe, Julai 31, 2018.

Polisi wa kuzuia ghasia wamepelekwa kwenye makao makuu ya chama cha upinzani cha MDC nchini Zimbabwe Jumatano.

Vyanzo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wafuasi wa chama hicho wanakilaumu chama tawala cha ZANU-PF kwa kujaribu kuiba kura za uchaguzi wa rais dhidi ya mgombea wao Nelson Chamisa.

Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa Jumatano na Tume ya Uchaguzi baada ya kuhesabu kura za majimbo 153, chama tawala cha ZANU- PF kinaongoza kwa viti 110 kati ya viti 210 vya bunge huku chama kikuu cha upinzani cha MDC kikiwa na viti 41.

Tume ya uchaguzi imesema kura za wagombea urais zinaendelea kuhesabiwa huku matokeo yakitarajiwa kutangazwa mapema wiki hii.

Kama ZANU-PF ikishinda angalau viti 30 za viti muhimu, itakuwa na theluthi mbili ya wingi jambo ambalo litawezesha kufanya mabadiliko ya kikatiba bila kuwa na kura za wabunge wengine ndani ya bunge.

XS
SM
MD
LG