Mugabe mwenye umri wa miaka 94 alijiuzulu kufuatia shinikizo la jeshi Novemba 2017, na nafasi yake kuchukuliwa na rais wa sasa Ermason Mnangawa mwenye umri wa miaka 75.
Kiongozi huyo wa zamani wa Zimbabwe amesema anaunga mkono mgombea wa upinzani wa chama cha- MDC, Nelson Chamisa mwenye umri wa miaka 40.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Jumapili kwenye mji wa Harare, Mugabe alisema hawezi kupigia kura wale waliomsababisha kuugua.
Wachambuzi wanasema uchaguzi wa safari hii umekuwa na wagombea wengi zaidi ambapo Mugabe ambaye ametawala kwa miaka 38 sio mgombea katika uchaguzi wa mwaka huu.
Wachambuzi wa kisiasa nchini Zimbabwe wanasema kuwa ingawaje Mnangagwa ameonyesha kuwa ni mgombea aliyoko mstari wa mbele katika ushindani, lakini kwa upande wa upinzani CHAMISA ameonyesha kuwa chaguo la wengi.