Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:49

Kenyatta asaini sheria ya mitandaoni


Watumiaji wa mitandao ya jamii nchini Kenya
Watumiaji wa mitandao ya jamii nchini Kenya

Rais Uhuru Kenyatta ametia saini sheria mpya ya makosa ya jinai ya mitandaoni iliyopitishwa na Bunge la Kenya 2017.

Sheria hiyo inaweka adhabu ya faini kubwa na kifungo cha jela cha muda mrefu kwa wale wanao wanyanyasa wengine na wanaoeneza habari za uongo kupitia mitandaoni.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Kenya, Sheria hiyo pia inawalenga waandishi wa habari, vyombo vya habari na watumiaji wa mitandao ya jamii, wenye blog na watumiaji wengine wa Inteneti.

Kutia saini huko kumefanyika wakati ambapo kumekuwa na wito kwamba rais airejeshe sheria hiyo Bungeni ili kuhakikisha vipengele vyake havikiuki katiba na kuvunja haki za uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujielezea.

Wiki iliyopita, Taasisi ya kuwalinda waandishi (CPJ) ilimtaka Rais Kenyatta kutosaini muswada huo uliopitishwa na bunge wakisema kuwa unakandamiza uhuru wa habari.

"Wabunge wa Kenya wamepitisha miswada kadhaa ambayo itafanya uhuru wa kujielezea kuwa ni kosa la jinai na kufanya waandishi wa habari na wanaomiliki blog kuwa wa kwanza kuathirika na muswada huo iwapo utasainiwa," alisema Mratibu wa CPJ Afrika Angela Quintal huko New York.

XS
SM
MD
LG