Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:43

Polisi wamwuita Mbunge Sugu kujibu madai ya uchochezi


Joseph Mbilinyi (Sugu)
Joseph Mbilinyi (Sugu)

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, nchini Tanzania, Ulrich Matei, amethibitisha Alhamisi kuwa jeshi hilo limemuita Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu, kujibu madai ya kutoa kauli ya uchochezi.

Kwa mujibu wa Kamanda Matei, Mbunge huyo ameonekana kulikosoa zoezi la kugawa vitambulisho maalum vilivyokuwa vimetolewa na Rais John Pombe Magufuli, kauli inayodaiwa na polisi kuashiria uchochezi, gazeti la Nipashe limeripoti.

Kamanda Matei amesema, "ni kweli tumemuita Mbunge Joseph Mbilinyi kwa mahojiano kutokana na maneno yake aliyoyazungumza kuhusu vitambulisho, maana tunaona kuna kukashifu, vile ni vitambulisho vilivyotolewa na serikali sasa tunapoona mtu anaanza kutoa maneno hayo, huo ni uchochezi"

Kamanda huyo pia alisema kuwa zoezi la kugawa vitambulisho lilikuwa na lengo zuri la kuwatambua wafanyabiashara hao.

Mapema wiki hii Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila alibainisha juu ya uwepo wa baadhi ya kauli zilizoashiria kudharau tukio la kugawa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo maarufu.

Disemba 2018 Rais Magufuli aliwakabidhi Wakuu wa Mikoa vitambulisho maalum kwa ajili ya kuvigawa kwa wafanyabiashara wadogo ili waweze kutambuliwa.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington , DC.

XS
SM
MD
LG