Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:40

Vyama 10 Tanzania vyapinga mahakamani muswada wa vyama vya siasa


Zitto Kabwe
Zitto Kabwe

Vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefunguwa kesi kupinga muswada wa vyama vya siasa kujadiliwa bungeni kwani unapingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vyama hivyo ni Chama cha ACT-Wazalendo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chama cha Kijamii (CCK), Chama cha Democratic Party ( DP), Chama cha NCCR MAGEUZI, National League for Democracy (NLD) na Chama cha United People's Democratic Party (UPDP).

Muswada huo ukipitishwa na kuwa sheria utazuia pamoja na mambo mengine vyama hivyo visifanye mikutano ya hadhara.

Lakini Zitto amesema vyama vya upinzani kwa kauli moja vimetoa tamko katika mkutano uliofanyika Zanzibar kwamba watafanya mikutano ya hadhara kwa sababu ni haki yao ya kikatiba.

"Tunajua kuwa uhuru haupatikani kwa kungojea kuupokea katika sahani ya fedha," amesema.

Ameongeza kuwa wanafahamu mikutano ya hadhara ambayo wataifanya 2019 itasababisha wapinzani kukamatwa, kupigwa, kufungwa.

Muswada wa sheria ya vyama vya siasa ulipelekwa Bungeni na Mwanasheria Mkuu wa serikali Novemba 2018 na unatarajiwa kujadiliwa bungeni Januari 29, 2019.

Amesema kesi hiyo ilifunguliwa Desemba 20 mwaka jana na itaanza kusikilizwa kwa mara ya kwanza kesho Ijumaa Januari 4, na imefunguliwa na yeye Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Naibu Katibu Mkuu Bara Chama cha Wananchi (CUF) Joram Bashange na Mkurugenzi wa habari, Uenezi na mawasiliano ya umma wa chama hicho Salim Abdalla Bimani kwa niaba ya vyama hivyo.

“Tumeamua kupeleka suala hili mahakamani kwa sababu waliolileta bungeni kwa mara ya kwanza walidai kuwa unaboresha sheria iliyopo sasa ya vyama vya siasa, lakini ukweli ni kuwa muswada huo umetungwa ili kufifisha Demokrasia hapa nchini, “ amesema Zitto.

Aidha mapungufu muswada huo kufanywa kuwa jinai matendo yanayo fanywa na vyama vya siasa, kutoa madaraka makubwa kwa msajili wa vyama vya siasa, kumpa kinga msajili wa vyama vya siasa na watumishi wa ofisi yake dhidi ya mashtaka na kuingilia uhuru wa vyama kuijiendesha.

XS
SM
MD
LG