Kwa mujibu wa wakili wake, Jebra Kambole polisi wameeleza hawawezi kumwachia kwani wanaendelea kumhoji, "hivyo hawawezi kumpa dhamana,"
Zitto alikamatwa na polisi Jumatano saa 5 asubuhi na kupelekwa kituo cha polisi Oysterbay, ambako alihojiwa kwa takribani saa tatu, kisha kuhamishiwa kituo kikuu cha polisi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Liberatus Sabas amewaeleza wanahabari kuwa wanamshikilia Zitto kutokana na matamshi aliyoyatoa hivi karibuni.
Jana, Jeshi la Polisi mkoani Kigoma lilimtaka Zitto kuwasilisha vielelezo juu ya kauli aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari Jumapili iliyopita Oktoba 28, 2018 kuwa ana taarifa za wananchi zaidi ya 100 kuuawa katika tukio la mapigano ya wananchi wa jamii ya Wanyantuzu na polisi wilaya ya Uvinza mkoani humo.