Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 15:42

Viongozi wa Chadema Tanzania warudishwa rumande


Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe

Mahakama Kuu imeahirisha Jumatano kesi inayowakabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime mjini Esther Matiko hadi Alhamisi kutokana na mwenendo wa kesi kutowasilishwa mahakamani.

Mbowe, Matiko na wenzao saba ambao ni viongozi wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania, wanakabiliwa na kesi ya jinai, Mahakama ya Kisutu, kwa mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi wa uasi. Mbowe na Matiko walirudishwa rumande.

Mahakama hiyo Ijumaa Novemba 23, 2018, iliwafutia dhamana Mbowe na Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana kwa kusafiri nje ya nje bila kibali cha Mahakama hivyo kushindwa kufika mahakamani siku ambazo kesi yao ilipangwa kwa usikilizwaji wa awali.

Uamuzi huo wa kuwafutia dhamana ulitolewa Ijumaa iliyopita kufuatia maombi yaliyotolewa na upande wa mashtaka, Novemba 12, 2018.

Wakili KIbatala

Kwa mujibu wa gazetl la Nipashe muda mfupi baada ya kufutiwa dhamana, washtakiwa hao kupitia kwa wakili wao, Peter Kibatala walikata rufaa Mahakama Kuu, kupinga uamuzi huo, huku wakiwasilisha jumla ya sababu nne za kupinga uamuzi huo, chini ya hati ya dharura.

Katika rufaa hiyo pamoja na sababu nyingine, walidai Mahakama ya Kisutu ilikosea kuwafutia dhamana bila kuwapa wadhamini wao taarifa ya kujieleza kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza.

Sababu nyingine walidai Mahakama ya Kisutu imekosea kuwafutia dhamana wakati walifika mahakamani wenyewe Novemba 12 bila kukamatwa na Ijumaa Novemba 23, 2018.

Vilevile walidai masharti ya dhamana aliyopewa ni kinyume cha sheria kwa kuwa hata mantiki au hata viwango vya kisheria.

Jaji Rumanyika

Jaji Sam Rumanyika anayesikiliza kesi ya pingamizi la rufani ya kupinga uamuzi wa kufutiwa dhamana kwa viongozi hao amepiga simu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiamuru mwenendo wa kesi na uamuzi uliowafutia dhamana washtakiwa hao umfikie ofisini kwake haraka.

Akipiga simu kwa karani wa mahakama baada ya kukosa namba ya Hakimu

Baada ya simu kupokelewa Jaji Rumanyika alijitambulisha kwa majina huku sauti ya upande wa pili (sauti ya karani Comas) ilisikika akiitikia kumfahamu.

Jaji Rumanyika alimuuliza kama anaifahamu kesi Namba 112/2018 naye akajibu anaifahamu, kisha akauliza kwanini nyaraka zilizomfikia hazijakamilika, hakuna uamuzi wa mahakama na mwenendo wa kesi.

Karani alijibu kwamba bado hazijamaliziwa kuchapwa na Jaji Rumanyika alitaka ampelekee hivyo hivyo ziwe zimechapwa au zimeandikwa kwa mkono.

“Nenda unileee nakusubiri ofisini kwangu chumba namba 16… Nasubiri, “Jaji Rumanyika ilikata simu na kuzitaka pande zote mbili kusubiri hadi saa saba wajiridhishe kupata nyaraka hizo.

XS
SM
MD
LG