Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:22

Tanzania : Lowassa arejea CCM


Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa wa pili kulia akipokelewa na Mwenyekiti wa CCM John Magufuli katika ofisi ndogo cha CCM Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa wa pili kulia akipokelewa na Mwenyekiti wa CCM John Magufuli katika ofisi ndogo cha CCM Dar es Salaam.

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, nchini Tanzania. Lowassa alikuwa mgombea wa kinyang’anyiro cha urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Uchaguzi mkuu 2015.

Kurejea kwa Lowassa kulikuwa kukitabiriwa na baadhi ya watu, lakini mara kadhaa Lowassa alikanusha kuwa anampango wa kurudi katika chama hicho.

Vyanzo vya habari vinasema hatua hiyo imewashitua watu wengi, kwa sababu ya kile ambacho kilisababisha yeye kuhama chama hicho.

Lowassa baada ya kuitumikia CCM kwa kipindi kirefu alikihama chama cha hicho kufuatia mvutano uliotokea baada ya kutoidhinishwa na chama hicho kuwa mgombea wa urais.

Sherehe za mapokezi yake wakati akirejea rasmi Ijumaa zilifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyoko Lumumba Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho John Magufuli.

Lowassa mara kadhaa amefanya mazungumzo na Rais John Magufuli, Ikulu ya Tanzania.

Kumekuwa na wimbi la wanachama wa upinzani kuingia CCM tangu Magufuli achaguliwe 2015, kitu ambacho kimekuwa kikizungumziwa katika duru za siasa kwamba kinadhoofisha upinzani.

XS
SM
MD
LG