Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:24

Edward Lowassa ahojiwa na polisi


Kiongozi wa upinzani, Edward Lowassa.
Kiongozi wa upinzani, Edward Lowassa.

Kiongozi mwandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa anashikiliwa na polisi Jumatatu katika Wilaya ya Geita.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari mjini Geita, Lowassa ambaye alikuwa mgombea urais katika kinyang’anyiro hicho mwaka 2015 amekamatwa kwa tuhuma za kuendesha mkutano bila ya ruhusa ya serikali.

Mmoja wa waandishi wa habari aliyekuwa katika tukio hilo ameiambia idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika VOA baada ya Lowassa kufika katika stendi ya zamani ya mji huo huku akiwapungia wananchi mkono akiwasalimia jeshi la polisi liliwasili ghafla na kumweka chini ya ulinzi.

Afisa wa polisi wa Geita, Ali Kitumbo aliyeongoza operesheni hiyo alisikika akisema kuwa Lowassa amefanya mkusanyiko wa watu bila ya kuwa na kibali.

Hata hivyo waandishi waliokuwa katika kituo cha polisi ambako mwanasiasa huyo anashikiliwa wamesema hawakupata fursa ya kuzungumza na polisi hao.

Lakini taarifa zinaeleza kuwa baada ya Lowassa kukamatwa wananchi walianza kupiga makelele na hali ya taharuki ilitokea.

Wananchi walisikika wakihoji "kwani Lowassa kuja kutusalimia wananchi tuliompa kura kuna kosa gani".

Lakini mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa polisi wanasema baada ya wananchi kufika polisi wakiwemo wanawake na wanaume walianza kupigwa na kuwekwa chini ya ulinzi.

Waandishi wawili waliokuwepo katika tukio hilo vifaa vyao vilivunjwa k, japokuwa waliachiwa huru.

“Hivi sasa tuko nje ya jengo la polisi tukisubiri mheshimiwa Lowassa aachiwe kwani bado yuko chini ya ulinzi na anahojiwa,” alisema mwandishi mmoja wao.

XS
SM
MD
LG