Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:51

Kigoda cha Mwalimu : Mjadala kuondoa hofu, chuki muhimu


Julius Nyerere, Rais wa zamani wa Tanzania akichangaya mchanga wa Zanzibar na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Julius Nyerere, Rais wa zamani wa Tanzania akichangaya mchanga wa Zanzibar na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mdahalo wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Ijumaa wenye anwani ya ‘Mienendo ya Uchaguzi na Mustakbali wa Mataifa ya Afrika umegusia hofu inayo wakabili wapiga kura Tanzania.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya (Chadema) na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amesema wananchi wamejazwa hofu inayo wafanya wachague watu ambao hawakuwapenda wakati wa uchaguzi.

Amesema alishangazwa kuona Landrover 45 za polisi zikiranda randa kwenye Jimbo la Monduli, wakati wa uchaguzi mdogo jambo ambalo alisema liliwatia hofu wananchi.

"Mimi naona nchini kuna tatizo la hofu na chuki. Inajengwa hofu kubwa sana kwa wananchi wakati wa uchaguzi. Pale Monduli tulifanya uchaguzi, kale kamji ni kadogo sana lakini kulikuwa na Landrover 45 za polisi na magari manne ya upupu, utafikiri kuna vita na hivi vinafanywa kutumia vyombo vya dola kusimamia uchaguzi," alisema.

Gazeti la Nipashe nchini limeripoti kuwa Lowassa alisema ni muda mwafaka nchi ikatazama utaratibu wa viongozi kuzungumza na wananchi ili kuondoa chuki na hofu.

Pia ametaka mambo yaliyo andikwa kwenye Rasimu ya Katiba iliyo andaliwa na Tume iliyo kuwa chini ya Jaji Joseph Warioba yafanyiwe kazi.

"Katiba ile ya Warioba kama wanasiasa wangekubali kushirikiana, ina mapendekezo ya wazee ambao wanaweza kuwaita viongozi wakawaambia kwamba hili na hili si sawa," alisema Lowassa.

"Chuki inakuwa mbaya sana ukiwa mwanachama wa CCM na mwenzako akiwa wa Chadema basi mchukiane, hii inatia hofu watu. Nchi hii imekuwa na amani na utulivu kwa miaka mingi sana. Tukiona mambo kama haya yanatokea tuchukue hatua," alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku, alisema ni vyema yakawepo mabadiliko ya Katiba kwa sababu wananchi hawaridhishwi na mambo yanayo endelea katika uchaguzi mbalimbali.

"Kila baada ya wananchi kupiga kura kuna kuwa na vurugu zinazo sababishwa na viongozi ambao wanajulikana lakini hakuna hatua zinazochukuliwa… ipo haja ya kuitizama Katiba Mpya ili kujirekebisha kutokana na mienendo ya uongozi uliopo,” alisema.

Alisema Katiba iliyo kubaliwa na wananchi na baadaye ikapelekwa kwenye Bunge Maalumu, ndio ina majibu ya maswali yote.

Naye Profesa Alexander Makulilo wa UDSM, alisema uchaguzi si njia pekee ya kuimarisha demokrasia bali ni njia ya kuondoa uongozi wa mabavu.

Kwa upande wake, Profesa Musambayi Katumanga kutoka Nairobi, Kenya alisema nchi nyingi za Afrika zinatumia fedha nyingi kwenye uchaguzi badala ya kunufaisha watu wake.

XS
SM
MD
LG