Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:37

Viongozi wa Chadema kula Pasaka rumande


Freeman Mbowe
Freeman Mbowe

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Alhamisi imewapa dhamana viongozi sita wa Chadema, ingawaje viongozi hao wataendelea kula Pasaka wakiwa Rumande.

Viongozi hao akiwemo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu (Bara) Dkt. Vicent Mashinji, John Mnyika (Mb) Salum Mwalimu (Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar) na Ester Matiko (Mb).wataletwa mahakamani kukamilisha masharti ya dhamana Aprili 3, 2018.

Taarfa za awali kutoka Mahakamani zilisema kuwa viongozi hao sita tayari walikuwa wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 20.

Akizungumza na waandishi wa habari Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari amelalamika kuwa inashangaza ni vipi mahabusu hao hawakuletwa mahakamani.

Amedadisi kuwa mahabusu wengine wengi walikuwa wameletwa na kutaka kujua magari matatu yaliyowachukua siku ya Jumanne kuwapeleka rumande yalikuwa yamekwenda wapi.

Wanasiasa hao hawakuletwa mahakamani kusikiliza dhamana yao wakati afisa wa magereza aliiambia mahakama kutokufika kwao na gari iliyokuwa iwalete mahakamani kuwa bovu.

Mahakama ilitoa masharti ya dhamana kwa kila mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili pamoja na ya shilingi milioni 20, sawa na takribani dola 9000 za kimarekani.

Pia Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ni miongoni mwa wanachama na viongozi wa juu wa Chadema waliofika kufuatilia mwenendo wa kesi inayowakabili Mbowe na viongozi wengine wa chama.

Wafuasi wa chama hicho pia walijitokeza wakiwa nje ya mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam wakisubiri uamuzi wa mahakama juu ya rufaa hiyo.

XS
SM
MD
LG