Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:48

Polisi wamnyima dhamana Halima Mdee wa Chadema


Halima Mdee
Halima Mdee

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amekamatwa na polisi jijini Dar es Salaam, Tanzania, Jumamosi kuhusiana na tuhuma za kutoa kauli ya kumkosea heshima Rais Magufuli.

Kamanda wa Polisi - Kanda maalum Dar es Salam, Lazaro Mambosasa, amesema Mwanasiasa huyo yuko mbaroni na sio kwamba ameitwa kuhojiwa kama inavyodaiwa na wakili wake Hekima Mwasipu.

Vyanzo vya habari vinasema Mwasipu amesema Mdee amehojiwa kwa muda wa saa mbili na kunyimwa dhamana.

"Polisi wamemhoji kwa masaa mawili kutokana na kauli aliyoitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mikocheni Februari 21, 2018," amesema wakili Hekima.

Katika mtandao wake wa twitter Halima Mdee ameandika kupitia Mtandao wake wa Twitter ameitwa na polisi lakini hakuambiwa anaitwa kwa sababu gani.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG