Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:10

ADB yaipa Afrika Kusini mkopo wa dola milioni 300 kukabiliana na COVID-19


Wafanyakazi wa afya wanasafisha hema linalotumika kuwatibu wagonjwa wa Covid-19, Hospitali ya Wilaya ya Tshwane, mjini Pretoria, Africa Kusini, Julai 10, 2020.
Wafanyakazi wa afya wanasafisha hema linalotumika kuwatibu wagonjwa wa Covid-19, Hospitali ya Wilaya ya Tshwane, mjini Pretoria, Africa Kusini, Julai 10, 2020.

Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) imeidhinisha mkopo wa dola milioni 300 kwa serikali ya Afrika Kusini ili kusaidia katika kupambana na janga la virusi vya corona na bajeti yake ya matumizi.

Uchumi wa Afrika Kusini ulikuwa tayari umedorora kabla ya janga la COVID-19 kuanza kuathiri vibaya uchumi wa taifa hilo.

Utabiri wa sasa unaonyesha pato la ndani litashuka kwa asilimia 7 mwaka huu, na nakisi ya bajeti itakuwa karibu asilimia 15 ya pato la jumla la taifa.

Afrika kusini ndio nchi yenye idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona barani Afrika, ikiwa na visa zaidi ya laki 3 na elfu 80.

Benki ya maendeleo ya Afrika ilisema katika taarifa kwamba mkopo huo ni wa kulinda Maisha ya raia wa Afrika kusini kwa kuhifadhi nafasi za ajira, na kuyasaidia makampuni katika uchumi rasmi na usio rasmi.

Afrika kusini iliwasilisha pia ombi la msaada wa fedha kwa shirika la kimataifa la fedha duniani IMF katika juhudi zake za kupambana na virusi vya corona. IMF inatarijiwa kutoa jibu kuhusu ombi hilo wiki ijayo.

XS
SM
MD
LG