Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:14

Baadhi ya nchi za Afrika zafunga mipaka na kusitisha safari za ndege kudhibiti maambukizi


Takwimu za maambukizo ya virusi vya corona Afrika.
Takwimu za maambukizo ya virusi vya corona Afrika.

Nchi kadhaa za Afrika zimefunga mipaka yake, kusitisha safari za ndege na kuzuia wageni kuingia, huku watu wanaodhaniwa kuambukizwa virusi vya Corona wakitakiwa kujitenga ili kuzuia virusi hivyo kusambaa.

Maambukizi ya virusi vya Corona yameripotiwa katika nchi 26 za Afrika na idadi ya maambukizi inaendelea kuongezeka.

Hadi sasa watu 22 wametengwa kwa uangalizi maalum nchini kenya baada ya kugunduliwa kukaribiana na wagonjwa wenye virusi vya Corona wanaoendelea kupokea matibabu katika hospitali za Mbagathi na Kenyatta jijini Nairobi.

Rais Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema nchi yake imepiga marufuku wageni kutoka nchi ambazo zimeripoti maambukizi ya Corona na kwamba raia wa Kenya pekee na wale walio na vibali sahihi vya kuishi Kenya, wanaruhusiwa kurejea nchini humo.

Wakati huohuo watu wanaorejea Kenya, wametakiwa kujitenga ili kuzuia maambukizi. Amri hiyo itadumu kwa muda wa siku 30.

Serikali ya Kenya pia imeagiza Shule na vyuo vikuu kufungwa wiki hii. Raia wamehimizwa kufanya ununuzi kwa kutumia kadi za benki au teknolojia kama kwa njia ya simu, badala ya kubeba pesa taslimu ambazo huenda zina virusi hivyo hatari.

Kenya imerekodi visa vitatu vya maambukizi ya Corona, huku Ethiopia ikiripoti visa vine, kufikia wakati tunaandaa ripoti hii.

Africa Kusini

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza hali ya dharura ya kitaifa nchin humo, na kuonya kwamba mlipuko huo huenda ukasababisha madhara makubwa kwa uchumi wa nchi.

Amepiga marufuku wageni kutoka nchi ambazo zimeripoti maambukizi kama Italia, Ujerumani, China na Marekani.

Rais Ramaphosa pia ametangaza marufuku ya watu kukusanyika kwa makundi ya zaidi ya watu 100. Afrika kusini imeripoti visa 61vya maambukizi ya Corona.

Maambukizi Itali

Italy imerekodi vifo vya watu 368 zaidi, kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

Idadi hiyo ni ongezeko kubwa nchini humo tangu ugonjwa huo ulipotokea, huku kukiwepo wasiwasi wa sekta ya afya ya nchi hiyo kuzidiwa na idadi ya maambukizi mapya.

Italy ni nchi ya pili Ulaya kuripoti kiwango cha juu cha maambukizi baada ya China ambako virusi hivyo vilianzia.

Waziri mkuu Giuseppe Conte, amesema serikali inajaribu kadri ya uwezo wake kupata vifaa vya kutosha kwa ajili ya kulinda raia wake dhidi ya maambukizi.

Conte amesema maafisa wanazingatia sana kusaidia watu katika eneo la Lombardy, kaskazini mwa nchi ambapo maambukizi makubwa yameripotiwa.

Jumla ya watu 24,747 wameambukizwa Corona nchini Italy, vifo 1,809 vikiwa vimeripotiwa.

Maambukizi ya Corona yameongezeka zaidi ulaya, katika siku za hivi karibuni.

Hatua za nchi mbalimbali

Viongozi wa nchi mbalimbali duniani wamepiga marufuku usafiri, kufunga shule, kutaka wafanyakazi kufanya kazi wakiwa nyumbani, kupiga marufuku mikusanyiko ya sherehe, michezo n ahata kidini, ili kukabiliana na virusi vya Corona.

Hatua hizo zinachukuliwa huku idadi ya maambukizi ikiendelea kuongezeka, anavyoripoti Abdushakur Aboud.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG