Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:24

Dunia yaadhimisha Siku ya kupambana na Ukimwi huku changamoto za Corona zikiongezeka


Bango linaloonyesha azima ya kutokomeza ukimwi kufikia mwaka wa 2030 likiwa katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa mjini Harare, Zimbabwe.
Bango linaloonyesha azima ya kutokomeza ukimwi kufikia mwaka wa 2030 likiwa katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa mjini Harare, Zimbabwe.

Leo ulimwengu unaadhimisha siku ya  ukimwi duniani, huku mashirika kote ulimwenguni yakisisitiza umuhimu wa kuwasaidia watu wanaoishi na HIV na kuathiriwa na virusi hivyo.

Pamoja na maadhimisho hayo, tarehe Mosi Disemba kila mwaka, pia ilitengwa na Umoja wa Mataifa kama siku ya kuwakumbuka waliofariki kutokana na ugonjwa huo.

Mwaka huu, siku hii inaadhimishwa wakati ulimwengu unakabiliwa na janga la virusi vya corona.

Shirika la umoja wa mataifa la kupambana na ukimwi(UNAIDS) linasema janga la corona limefanya iwe vigumu sana kwa watu wanaoishi na HIV kupata huduma za afya na huduma nyingine, likisisitiza pia juu ya ukosefu wa usawa pamoja na hali ya unyayapaa.

Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mjini Capetown, Afrika Kusini.
Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mjini Capetown, Afrika Kusini.

UNAIDS imetoa wito kwa serekali kuongeza uwekezaji na kuchukua hatua dhidi ya ukimwi na majanga mengine.

Umoja wa mataifa unasema mifano inaonyesha kuwa kutakuwa na ongezeko la maambukizi mapya ya HIV laki 1 na elfu 23 hadi laki mbili na elfu 93 na kati ya vifo elfu 69 na laki moja 1 elfu 48 kutokana na ukimwi ifikapo mwaka wa 2022, hasa kwa sababu janga la corona limeathiri juhudi za kupambana na HIV.

Kwa watu millioni 38 wanaoishi na HIV ulimwenguni kote, millioni 26 kati yao wanatumia dawa za kupunguza makali ya ukimwi. Mwaka 2019, watu laki 6 na elfu 90 walifariki kutokana na maradhi yanayohusishwa na ukimwi.

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kupewa msaada wa dola billioni 35 ili utowe msaada wa kibanadamu wa kuokoa maisha ya watu millioni 160 mwaka ujao, wakati madhara ya kiuchumi yaliosababishwa na janga la virusi vya corona yalipelekea ma millioni ya watu ulimwenguni kujikuta katika hali mbaya ya umaskini.

‘’Mizozo, mabadiliko ya hali ya hewa na covid 19 vimesababisha changamoto kubwa ya kibinadamu tangu vita vya pili vya dunia”, katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guteress amesema wakati wa uzinduzi wa wito huo.

Amewaomba wafadhili kusaidia wale ambao maisha yao yako hatarini.

Umoja wa mataifa unasema watu millioni 235 au mtu mmoja kati ya watu 33 duniani anahitaji msaada au ulinzi.

Visa millioni 63 vya maambukizi ya virusi vya corona vimethibitishwa ulimwenguni kote kulingana na takwim za chuo kikuu cha marekani, John Hopkins. Watu millioni 1 na laki 5 walifariki kutokana na ugonjwa huo, huku ma millioni ya wengine wakipoteza ajira wakati wa masharti magumu yaliochukuliwa na serekali tofauti kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

-Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG