Aina mpya ya virusi vya Corona vinavyosambaa kwa kasi sana kuliko aina ya kwanza, imegunduliwa katika nchini za Botswana, Zambia, Gambia na Kenya.
Mkurugenzi wa shirika la afya duniani katika bara la Afrika Matshidiso Moeti, amesema kwamba virusi hivyo vinasambaa kwa kasi kutokana na safari nyingi za watu kote Afrika.
Katika kikao na waandishi wa habari, Matshidiso amesema kwamba mpango wa COVAX, wa shirika la afya duniani unaolenga kutoa chanjo kwa nchi maskini, unapanga kutoa dozi milioni 600 dhidi ya virusi vya Corona kote Afrika ifikapo mwaka 2021.
Amesema kwamba watu milioni 3.3 wameambukizwa virusi vya Corona kote Afrika kufikia sasa.
Afrika kusini ndio nchi ya Afrika ambayo imeathirika zaidi kutokana na janga la Corona Afrika.